Diamond na Ommy Dimpoz kwenye pozi
Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
WASANII mahiri wa miondoko ya kizazi kipya nchini Tanzania, Naseeb Abdul ‘Diamond’ na Ommy Diampozi,
wanatarajia kupanda jukwaani kutoa burudani katika Sikukuu ya Krismasi, kwenye
Ukumbi wa Dar Live, uliopo Mbagala, Zakheem jijini Dar es Salaam.
Diamond na Dimpoz,
watakutana kwa mara ya kwanza katika ukumbi huo, ikiwa ni kusherehekea pamoja
na wadau wa muziki huo pamoja na mapambano ya ngumi.
Onyesho hilo maalum la
kusherehekea Krismasi, limeandaliwa na Kampuni ya Global Publishers na
Oganaizesheni ya Ngumi za Kulipwa nchini (TPBO), chini ya Rais wake, Yasin
Abdallah ‘Ustadhi’.
Akizungumza kuhusu
onyesho hilo, Diamond alisema ni faraja kwake kujumuika na mashabiki wake
katika ukumbi wa Dar Live na kuwapa burudani, huku akiwaomba kujitokeza kwa
wingi katika onyesho hilo.
“Kwanza nawashukuru
mashabiki wangu wa kuniunga mkono na kununua kazi zangu, nawaomba mjitokeze kwa
wingi Dar Live, mshuhudie nitakavyomfundisha kazi mdogo wangu Diampoz, mimi ni
kaka yake na aliyetangulia katangulia tu,” alisema Diamond huku akishangiliwa
na masjhabiki waliofurika nje ya viwanja vya Karume, Dar es Salaam.
Katika onyesho hilo pia
kutakua na mapambano ya ngumi, ambapo bondia Mbwana Matumla wa Tanzania,
atazichapa na David Charanga kutoka Kenya, katika pambano la raundi 6, huku
Mada Maugo wa Tanzania, akizichpa na Yiga Juma kutoka Uganda katika pambano la
raundi 6 pia.
Katika pambano jingine,
Chupaki Chipinda, atazichapa na Bahati Mwafyele katika pambano la raundi 6, aambapo
pia kutakua na burudani kutoka kwa kundi la muziki wa dansi la Extra Bongo,
pamoja na msaniii wa Kizazi Kipya kutoka TMK Wanaume, Juma Nature.
Katika onyesho hilo la
aina yake, kiingilio kitakua Sh 10, 000.
No comments:
Post a Comment