Madee kushoto akiwa na dogo Janja
Na Kambi Mbwana, Dar
es Salaam
KUIBUA au kusimamia wasanii wachanga, wakati mwingine kunahitaji
moyo wa chuma. Ni kutokana na baadhi yao
kushindwa kukubali wala kukumbuka fadhila, jambo ambalo ni magumu matokeo yake.
Matokeo yake ni magumu kiasi cha kuwaumiza vichwa wengine,
wale waliokuwa na nia njema na watu ambao kwa hakika, wametumia muda na gharama
kubwa.
Chid Benz, mkali wa michano Tanzania
Nimelazimika kusema hili baada ya kusikia na kuona maneno ya
msanii chipukizi wa muziki wa Hip Hop, Abdulimalick Chande maarufu kama Dogo Janja, alivyoweza kumjia juu mkombozi wake
kisanaa, Ahmad Ally Madee.
Nasema hivyo baada ya kuona kwamba Dogo Janja, amebwatuka,
kupayuka juu ya Madee ambaye ndiye aliyefanya juhudi ili awe juu.
Sitaki kukubali kwamba Dogo Janja alikuwa anaibiwa au
kudhulumiwa na Madee na kundi lake la Tip Top ‘Connection’ lenye maskani yake
Manzese.
Nasema hivyo maana naelewa vizuri soko la muziki lilivyokuwa
hapa nchini. Najua zipo fedha zinazoingia, hasa za maonyesho, kama
walivyokuwa wasanii wengine.
Sio siri, Dogo Janja anaimba muziki wa Hip Hop ambao soko lake ni
gumu mno. Ni wachache wanaotamba, ndio maana hata shoo zao sio nyingi.
Ukiangalia kwenye
ramani ya muziki huo wa kizazi kipya, wasanii wa kuimba, iwe zouk, rhumba,
R&B ndio wanaotamba, kiasi cha mapato yao
kuwa mengi.
Sio Dogo Janja. Bado, kwanza ni mdogo kiumri ni kisanaa pia.
Dogo Janja, fedha zake sio nyingi, maana hata zile shoo za usiku hazipati.
Dogo Janja, nyimbo
zake ni tatu tu, ukiwamo ule wa ‘Anajua’ aliyoimba sambamba na nahodha wa kundi
lake la Tip Top, Tunda Man.
Kwa mujibu wa
sheria, Dogo Janja hawezi kufanya shoo za usiku, hasa za vinywaji vya pombe.
Huo ndio ukweli,
hivyo tunapojaribu kuliangalia sakata lake juu
ya Madee, aliyemuibua, tuwe makini.
Mimi kama mdau wa
muziki, niliwahi kuzungumza mengi na msanii huyo kabla hata ya kuwa maarufu kwa
asilimia chache.
Ndoto, mawazo
mengi yaliongozwa na moyo wa dhati wa kundi lake, linaloongozwa na Madee. Leo
Dogo Janja amesahau kiasi cha kumtusi mkubwa wake?
Kwa mujibu wa Dogo
Janja, ameamua kurudi kwao Arusha, maana Madee alimuibua ili amuibie. Hapa
utacheka. Maana anaongea bila kujua.
Hivi kama Dogo
Janja leo analalama kuibiwa, vipi jana alipokuwa akitumia fedha za watu,
kuandaliwa kisanaa hadi kwennda studio.
Vipi pale gharama
za kumtangaza zilipochukua nafasi yake ili awe maarufu na kufahamika? Mnyonge
mnyongeni lakini haki yake mpeni.
Kama wapo waliokuwa na nia
njema na Dogo Janja, ilikuwaje wasubiri hadi aendelezwe kipaji chake na Madee,
chini ya Meneja wa kundi lake, Babu Tale na Abdu Bonge.
Hili nalo linahitaji
elimu ya Chuo Kikuu kubaini kwamba sio kukosa shukrani tu, bali amekurupuka juu
ya kumtusi muungwana wake.
Ndio, maana ugumu wa sanaa ni kutoka tu. Kila mtu ni msanii
na ana nyimbo nzuri kuliko wanaojulikana. Ila wanashindwa jinsi ya kutoka na
kujulikana.
Sasa kama hivyo
ndivyo, kwanini tusiheshimu mchanngo wa wenzetu katika maisha yetu kisanaa?
Kwanini Bongo Fleva ni wapayukaji?
Ama kwakuwa wengi wao wanaendeshwa na vilevi? Na hawa ndio
wanaojifanya marafiki wa kweli kwa vijana wetu, ambao nao huwaamini
Sawa, ila kabla ya kupewa maneno ya kuwadharau wakombozi
wetu, ni vizuri tukatumia muda huo walau robo tu, kukumbuka tulipotoka.
Kwa mfano mimi. Mafanikio yangu, au kujua kwangu kwa kiasi
kidogo kuandika, hakika wapo au yupo ambaye amechangia kuniweka hapa.
Sasa itakuwa ujinga, wendawazimu kutembea hadharani na
kumtukana, kwa sababu tu, tumeshindwa kuelewana katika baadhi ya mambo.
Nafikiri hili ni jambo la busara na lazima liangaliwe upya
na wasanii wetu. Tuweke mbele hekima, maana sanana ipo na wakali wanazaliwa.
Aina hiyo ni kuwafanya wengine washindwe kusaidiwa kama wewe ulivyosaidiwa? Tatizo sio kuondoka kwenye
kundi, tatizo ni kutoa lugha za matusi, jambo linaloniumiza na kunichukiza na aina hii ya maisha ya wasanii wa
Tanzania.
0712 053949
0753 806087
No comments:
Post a Comment