Rachel wa THT akiwa jukwaani akifanya vitu vyake
Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
MKALI wa muziki wa kizazi kipya hapa nchini, Winfirda
Josephat maarufu kwa jina la 'Rachel wa THT', amesema kiuno chake kinawafanyua
madume wamsumbuwe kila wakati, jambo analopambana nalo kwa kiasi kikubwa.
Katika nyimbo zake nyingi, ukiwamo ule wa 'Kizunguzungu' na
sasa 'Nashukuru Umerudi' msanii huyo anafanya vitu vya aina yake, hasa kwa
kunengua na kubinua macho yake, kama ilivyokuwa kwa msanii Ray C.
Rachel aliiambia Handeni Kwetu kuwa mauno yake yanawatoa
udenda watu wenye matamanio, ingawa anakili kuwa usumbufu huo anakabiriana nao
kwa spidi 120.
Alisema kwamba amekuwa akiwaza kitu kimoja tu ambacho ni
muziki, hivyo wanaomtamani wafikirie zaidi kazi zake na sio mengineyo, hasa
anapokuwa nje ya Dar es Salaam kwenye ziara zake za kikazi zaidi.
“Midume inatoa macho kwa mauno yangu, lakini ninachoangalia
ni kazi yangu tu, hivyo hilo nimeamua kuliangalia kwa kina, ingawa naamini hao
nao ni mashabiki wangu na wanapenda kipaji changu.
“Naamini nitafika mbali zaidi kwa kuhakikisha kuwa nina kazi
nzuri na kuwapa burudani kamili mashabiki wangu katika shoo zote za ndani na
nje ya Dar es Salaam, ukizingatia kwamba hiyo ndio ajira yangu na naamini mambo
yatatakuwa mazuri,” alisema.
Recho kama anavyopenda kujiita anatokea katika taasisi ya
kulea na kukuza vipaji ya Tanzania House of Talents (THT), iliyoibua wasanii
wengi wenye uwezo wa kutisha, akiwamo Linah, Barnabas, Amini na wengineo.
No comments:
Post a Comment