Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
MWANAMUZIKI
na mmoja wa wakurugenzi wa bendi ya Mapacha Watatu, Jose Mara, ameipa masharti
bendi yake ya FM Academia, Wazee wa Ngwasuma kwa kuhakikisha kuwa hawaondoi
picha yake kwenye mabango yanayoitangaza Ngwasuma, ingawa yupo nje ya bendi
hiyo nchini.
Jose Mara
kwa sasa ameondoka Ngwasuma na kufanya kazi na Mapacha Watatu, akiwa sambamba
na Khalidi Chokoraa, huku wakiwa na pengo la Kalala Junior.
Akizungumza kwa hisia kali, Mara alimwambia mmoja wa mabosi wa Ngwasuma kuwa, sitaki nione mnaondoa sura yangu kwenye mabango yenu vinginevyo hata kuja kwenye shoo yenu itakuwa mwisho wangu,” alisema mwanamuziki huyo.
Ingawa
Mara alisema kama utani, lakini sura yake ilitangaza ukweli halisi, hasa
ukizingatia kwamba tangu aondoke kwenye bendi hiyo, lakini vipeperushi na
mabango yanayotangaza kikosi cha maangamizi hakijabadilishwa kwa kiasi kikubwa.
“Hili
bango nalipenda na kama siku nikiona limeondolewa basi utakuwa mwisho wangu
kuja kwenye shoo ya Ngwasuma,” alisema Jose Mara, akilizungumzia bango
lililowekwa nje ya New Msasani Club.
Jose Mara
ni miongoni mwa vijana mahiri wa muziki wa dansi hapa nchini, akitokea kuwa na
mashabiki wengi hapa nchini. Pia ni mmoja wa vijana wenye sauti jambo
lililomfanya apate namba kila wimbo wa FM Academia, maarufu kama Wazee wa Ngwasuma.
Zipo
habari zinazosema kuwa mwanamuziki huyo huenda akarudi Ngwasuma wakati wowote
kutokana na maisha ya Mapacha Watatu kuwa ya kusua sua, hasa baada ya Kalala
Junior naye kuamua kurudi Twanga Pepeta.
No comments:
Post a Comment