Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
MALKIA wa Mipasho nchini, Khadija Kopa na kundi lake cha Tanzania One Theatre (TOT)leo kitatoa shoo kabambe kusherekea sikukuu ya Krismas kwa wakazi wa Kata ya Kivule, Ilala kusherekea sikukuu ya Krismas kwenye ukumbi wa Vegetable Garden Pub.
Akizungumza
mapema leo asubuhi, Kopa alisema kikundi hicho ambacho kitamba na nyimbo kemkem
za taarab zinazotingisha katika miundoko ya Pwani ukiwemo Full Stop, Stop in
Town na Mjini Chuo Kikuu ameahidi kukonga nyoyo za mashabiki wake.
Alisema TOT
taarab imesheheni kila idara ikiwa na wanamuziki wenye uwezo mkubwa wa kupiga
taarab yenye mahadhi yanayokubalika akiwepo mkongwe Abdul Misambano, Mwanamtama
Amir, Ali Star, Rukia Juma na Kopa Junior anayeimba nyimbo za Omar Kopa.
Mkurugenzi
wa Vegetable Garden Pub, Anicety Mkwaya alisema maandalizi ya burudani hiyo
imekamilika na zawadi zitatolewa kwa wale watakacheza taarab vizuri na
watakaovaa vizuri.
Alisema
burudani katika ukumbi huo zinaendelea ambako Januari 29 bendi ya Msondo Ngoma
itatoa burudami katika ukumbi huo.
No comments:
Post a Comment