Picha mbalimbali za burudani ya Chagga Day Moshi
Ommy Dimpozi, akitoa shoo Chagga Day Festival
Na
Mwandishi Wetu, Moshi
TAMASHA
la Chagga Day Festival limefanyika kwa mafanikio makubwa katika Ukumbi wa Zumba
Landa, uliopo Moshi, Desemba 22, huku waandaaji wakifurahia na kuwapongeza
wadau wote waliofanikisha shughuli hiyo.
Tamasha
hilo kwa ujumla
lilipendeza huku likiandaliwa na kampuni hiyo ya burudani kwa ajili ya
kuwapatia burudani kamili watu wa huko sambamba na kuenzi mila na destuli za
kabila la Wachaga walioenea katika mkoa huo.
Mkurugenzi
wa Kampuni ya My Way Entertainment, Paul Maganga, aliwapongeza mashabiki na
wadau wote waliohudhuria kwa wingi kwenye tamasha hilo la Chagga Day Festival,
ambalo ni mwendelezo wa lile la kwanza la Chagga Day Cultural Festival 2012 -
Dar lililofanyika viwanja vya Leaders jijini Dar es Salaam miezi miwili
iliyopita.
Tamasha
hilo lilipambwa
na burudani ya muziki wa dansi toka kwa Serengeti Band yenye maskani yake
jijini Arusha, pamoja na kundi la madansa la Boda 2 Boda, bila kusahau nyota wa
muziki wa Bongo Fleva, Ommy Dimpoz.
Tamasha
hilo
lilidhaminiwa na TBL, TDL na SBC ambapo TBL ni kupitia bia ya Safari na SBC
wakisherehesha kupitia soda za PEPSI na TDL kupitia Konyagi.
No comments:
Post a Comment