Francis Cheka
Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
BONDIA wa ngumi za
kulipwa nchini, Francis Cheka, amepangwa kurudiana na Chiotra
Chimwemwe wa Malawi, Januari 26, nchini Ethiopia.
Pambano hilo litapigwa katika
jiji la Adddis Ababa, likitoa picha na kutangaza makali ya Mtanzania huyo,
mwenye asili ya mkoani Morogoro kasoro bahari.
Akizungumzia juu ya
pambano hilo, Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa
nchini (TPBC), kwa kupitia Rais wake, Onesmo Ngowi, alisema pambano hilo litafanyika mara
baada ya kumalizika lile la jijini Arusha, lililopangwa kufanyika Desemba 26.
Alisema Cheka na Chimwemwe watakutana jijini Arusha Desemba 26 (Boxing
Day) katika mpambano wa kutafuta nani mbabe wa uzito wa Super Middle
katika bara la Afrika, Mashariki ya Kati na Ghuba ya Uajemi (IBF AMEPG).
“Katika mpambano huo mafahali hawa wawili wataumana
kiume kwa raundi 12 za dakika tatu kila mmoja kwa ajili ya kuonyeshana umwamba,”
alisema Ngowi.
Umaarufu wa wawili hawa umewafanya mapromota
wanaoandaa tamasha la kuchangisha pesa kwa ajili ya kulisha watu wenye njaa
katika bara la Africa kuwaingiza Cheka katika
patashika hiyo.
No comments:
Post a Comment