https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543


Recent Post

Friday, April 06, 2018

Wazanzibar waaswa kuwa wazalendo na nchi yao

Na Mwandishiwetu, Zanzibar
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi  Dkt. Ali Mohamed Shein  amewaasa vijana wa Zanzibar kuwa Wazalendo na nchi yao  kwa kuisoma na kuijua historia ya Zanzibar ikiwa ni pamoja na kuenzi mchango wa Mwasisi wa Taifa hilo Hayati Sheikh Abeid Amani Karume.

Dkt. Shein  ameyasema hayo wakati akitoa hotuba ya ufunguzi katika  kongamano la kwanza la kumbukumbu ya Rais wa kwanza wa Zanzibar na Mwenyekiti wa kwanza wa Baraza la mapinduzi Hayati Sheikh Abeid Amani Karume,  lililofanyika katika Chuo cha kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere   katika kampasi ya Zanzibar, iliyopo Bububu  mjini Magharibi siku ya Alhamis tarehe 5 April, 2018.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi  Dkt. Ali Mohamed Shein akitoa hotuba ya ufunguzi wakati wa kongamono la kumbukumbu ya hayati sheikh abeid amani karume lililoandaliwa na chuo cha kumbukumbu ya mwalimu nyerere kampasi ya zanzibar.


“Hayati Sheikh Abeid Amani Karume,   alikuwa ni mtu mvumilivu na mstahimilivu, aliyeipenda Zanzibar na wananchi wake, hivyo ni vyema mchango wake katika kuleta maendeleo ya Zanzibar ukakumbukwa na kuenziwa.

Rais Karume ametumia fursa hiyo pia kukipongeza Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere kwa kuona umuhimu wa kuandaa Kongamano hilo ambalo ni la kwanza kufanyika visiwani Zanzibar.

Mikoa na wilaya zaagizwa kutenga maeneo ya hifadhi

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla, Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga,Zainab Telack na Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri wakipanda mti wa kumbukumbu wakati wa kilele cha kuadhimisha siku ya upandaji miti kitaifa iliyofanyika jana katika kijiji cha Mhunze wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga.

Na Hamza Temba, WMU, Kishapu, Shinyanga

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla amewaagiza Wakuu wa Mikoa nchini kuhakikisha Halmashauri zote nchini zinatenga maeneo katika kila kijiji kwa ajili ya uhifadhi wa misitu ikiwa ni pamoja na vijiji hivyo kuunda kanuni na taratibu zao wenyewe za kusimamia maeneo hayo.

Ametoa agizo hilo jana katika kijiji cha Mhunze wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga wakati wa kuhitimisha kilele cha Maadhimisho ya Upandaji Miti Kitaifa yaliyofanyika mkoani humo kuanzia Aprili 03 mwaka huu.

Muriya: Makazi yetu Oman ni fursa za kiuchumi kwa watu wote

Makazi ya Jebel Sifah nchini Oman ni fursa za kiuchumi kwa watu wote

Balozi Mdogo wa Oman Visiwani Zanzibar, Ahmad Mohamed Al Muzaini wa nne kutoka kulia akiwa amesimama baada ya kumaliza kuzungumza kwenye maonyesho ya makazi ya Oman Visiwani Zanzibar yakiandaliwa na Kampuni ya Muriya yenye maskani yake nchini Oman. Maonyesho hayo yamefanyika katika Hoteli ya The Park Hyatt, Zanzibar. Wengine ni wadau wa ardhi na makazi waliohudhuria kwenye maonyesho hayo. Picha na Mpiga picha wetu.

Na Mwandishi Wetu, Zanzibar
HUKU maonyesho ya makazi ya Jebel Sifah yanayoonyeshwa na Kampuni ya Muriya yenye maskani yake nchini Oman yakiendelea visiwani Zanzibar katika Hotel ya The Park Hyatt, baada ya kumalizika jijini Dar es Salaam, wafanyabiashara wa visiwani hapa wametakiwa kupanua wigo wao wa kibiashara kwa kununua makazi yao nchini Oman ili wajiwekee vitega uchumi kwa ajili ya maendeleo yao.

Ushauri huo umetolewa leo na Meneja Mauzo wa Muriya, Ghizlane El Gouchi, wakati wa kuelimisha wakazi na wananchi wa Zanzibar juu ya utendaji kazi wao katika sekta ya ardhi na makazi waliyojikita nchini Oman, huku wakijivunia maendeleo makubwa kwenye sekta hiyo muhimu dunian kote.

Tuesday, April 03, 2018

Watanzania waaswa kuchangamkia makazi nchini Oman

Meneja Mauzo Mwandamizi wa  Kampuni ya Ujenzi wa Makazi ya Muriya, Ghizlane El Gouchi (wa pili kushoto) akiwaonyesha wageni waliohudhuria hafla ya kuitambulisha kampuni hiyo kuelekea maonyesho ya biashara yaliyoanza leo jijini Dar es Salaam hadi Aprili 5 na Zanzibar Aprili 6. Kushoto ni Mshauri wa Mradi Mona Abel Malak, mshauri mwandamizi, Faisal Alzakwani,Mshauri Hamad Al Balushi na mshauri mwingine Omar Saleh. 

NA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM
Watanzania wameaswa kuchangamkia nyumba zinazouzwa na Kampuni ya Muriya yenye maskani yake Muscat nchini Oman, ili kujiweka katika kundi sahihi la kibiashara sanjari na kujipatia maendeleo makubwa kutoka kwa nchi ya Tanzania na Oman.

Hayo yamesemwa leo na Meneja Masoko na Kampuni ya Muriya Ghizlane El Gouchi, wakati anazungumza na waandishi wa habari katika maonyesho ya nyumba zinazouzwa na kampuni yao huku maonyesho hayo yakifanyika jana katika Hotel ya Hyatt Regency, jijini Dar es Salaam na kuhudhuliwa na watu mbalimbali wenye ndoto za uwekezaji wa majengo.

Saturday, January 13, 2018

Watanzania wanaoishi Saudi Arabia washerehekea Sikukuu ya Mapinduzi Riyadh Palace Hotel na Balozi Mgaza

Baadhi ya Watanzania wakiwa katika picha ya pamoja na Balozi Mgaza katikati mwenye suti.

Na mwandishi maalum, Riyadh - Saudi Arabia
Wanadiaspora na Watanzania waishio Riyadh nchini Saudi Arabia walisherehekea na kuandhimisha miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar  siku ya ijumaa tarehe 12 Januari, 2018 katika ukumbi wa Riyadh Palace Hotel. 

Sherehe hizo zilindaliwa na jumuiya ya Watanzania 'Tanzania Walfare Society' ambapo waalikwa mbalimbali kutoka miji ya Riyadh, Qasim na maeneo ya karibu walihudhuria. Mgeni rasmi katika sherehe hiyo alikuwa Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia, Mhe. 

Hemedi Mgaza. Miongoni mwa walihudhuria sherehe hizo pia walikuwa wanafunzi wa vyuo vikuu, wafanyakazi wapya wa kampuni ya ufugaji ng'ombe wa Maziwa ya Al Marai na wengine kutoka kampuni ya ufugaji kuku ya Al Watania.  Kwa picha na habari zaidi angalia kupitia you tube 'Prince eddycool'
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Watanzania ya Riyadh, Bw. Fuad Mabruk akitoa hotuba mbele ya Watanzania na wanadiaspora wa mji wa Riyadh huku nyuma yake walioketi kwenye meza kuu kuanzia kulia ni Makamu wa Mwenyekiti wa Jumuiya Dkt. Mahmoud Tuli, Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia Mhe. Hemedi Mgaza, Afisa Mkuu wa Utawala wa Ubalozi Bw. Ahmada Sufiani, Katibu wa Jumuiya ya Watanzania Bw. Saeed Al Jabry na wa kwanza kushoto ni Mweka Hazina wa Jumuiya Bw. Mohamed Saeed.
 Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia, H.E Hemed Mgaza, akizungumza na Watanzania.
Baadhi ya Watanzania na wanadiaspora wakisikiliza hotuba zilizokuwa zikitolewa na baadaye walipata fursa ya kuuliza maswali na kutoa maoni.

Friday, December 29, 2017

Watanzania wanaoishi Saudi Arabia wakutana kwa majadiliano
Kutoka Kushoto  Afisa Utawala wa Konseli Kuu ya Jeddah Ali Mohamed, Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia Mhe. Hemedi Mgaza, Spika Mstaafu wa Baraza la Wawakilishi Zanziabar Mhe. Pandu Amir Kificho ambaye alikuwa mgeni mwalikwa, Kaimu  Mwenyekiti wa Jumuiya ya Watanzania waishio mji wa Jeddah Bw. Salim Ali Shatri.
Baadhi ya Watanzania na wanadiaspora wa Jeddah wakiwa katika picha na meza kuu baada ya mkutano.

Na Mwandishi Maalum, Saudi Arabia
Jumuiya ya Watanzania waishio Jeddah nchini Saudi Arabia ' Tanzania Welfare Society' hivi karibuni ilifanya Mkutano wa pamoja wa wanajumuiya Watanzania na Wanadiaspora. Mkutano huo pia ulihudhuriwa na Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia Mhe. Hemedi Mgaza. Aidha, mkutano huo ulihudhuriwa na Spika Mstaafu wa Balaza la Wawakilishi Zanzibar Mhe. Pandu Amir Kificho ambaye alikuwa mgeni rasmi. Mhe. Pandu Amir Kificho alikuwa nchini Saudi Arabia kutekeleza ibada ya 'Umrah' katika miji ya Makkah na Madina.

Wanajumuiya walipata fursa ya kusikiliza hotuba zilizotolewa na Balozi na Spika Mstaafu wa Balaza la Wawakilishi. Vile vile waliweza kuuliza maswali na pia kutoa maoni na ushauri. 
Katika hotuba zilizotolewa wanajumuiya walisisitizwa kuwa na umoja na uzalendo kwa Tanzania. Walitakiwa kufanya kazi kwa bidii na kuhakikisha wanachangia maendeleo ya Tanzania. Habari zimeletwa na Mwandishi Maalumu wa Jeddah, Saudi Arabia. Kwa Picha na matukio mengine zaidi angalia youtube kupitia 'Prince eddycool' 
Watanzania na Wanadiaspora wa Jeddah wakisikiliza hotuba katika hoteli ya Trident.

Wednesday, December 13, 2017

Serikali yaipongeza Bikosports kuijaza mapesa Stand United


*Waziri Mwakyembe asema mpira ni pesa
*Ataka wadau wengine wawekeze

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
SERIKALI kupitia Wizara ya Habari, Sanaa, Michezo na Utamaduni, chini ya Waziri wake, Mheshimiwa Dr Harrison Mwakyembe, ameipongeza Kampuni ya Bikosports kwa kitendo chake cha kuidhamini timu ya Stand United ya Shinyanga kwa Sh Milioni 100.
Waziri wa Habari, Sanaa, Michezo na Utamaduni, Mheshimiwa Harrison Mwakyembe, akiangalia jezi yake aliyokabidhiwa na wadhamini wa klabu ya Stand United ya Shinyanga, Bikosports, wakiwa kwenye tukio la klabu hiyo kukabidhiwa hundi ya Shilingi Milioni 100 kama sehemu ya udhamini kwao. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Bikosports, Charles Mgeta, akiwa sambamba na Mbunge wa Shinyanga Mheshimiwa Steven Masele na kulia ni Mwenyekiti wa Stand United, Dr Ellyson Maeja.

Serikali imetoa kauli hiyo leo katika makabidhiano ya hundi ya Sh Milioni 100, yaliyofanyika katika Ukumbi wa Akemi na kuhudhuriwa na baadhi ya viongozi wa serikali, viongozi wa TFF na wadau wengine muhimu wa michezo.

Akizungumza katika tukio hilo, Waziri Mwakyembe alisema duniani kote mpira ni pesa, hivyo kitendo cha Kampuni ya Bikosports kuamua kuidhamini Stand kutachochea ari ya mafanikio katika nyanja ya mpira wa miguu nchini.

"Serikali inawapa hongera Bikosports kwa kuingia kwenye mpira wa miguu, hivyo ni matumaini yetu nitaongeza wigo wenu wa udhamini sanjari na kuingia pia kwenye klabu nyingine, tukiamini sasa mpira utachezwa uwanjani, hivyo Stand United lazima waitumie vizuri fursa ya kupata mdhamini," Alisema.

Wednesday, November 29, 2017

Halmashauri zaagizwa kutumia mafundi wa kawaida kwenye maeneo yao

Na Mwandishi Wetu, Mkalama
Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) Joseph Kakunda ameziagiza halmashauri zote nchini kutumia mafundi wa kawaida wazawa waliopo katika maeneo yao katika miradi yote midogo kupitia utaratibu unaojulika kama ‘force account’.

Naibu Waziri Kakunda ametoa agizo hilo jana mara baada ya kufanya ziara Wilayani Mkalama kufuatilia utoaji wa huduma mbalimbali kwa jamii huku akijikita zaidi katika sekta ya Maji na Elimu, ambapo ametembelea mradi wa maji Iguguno na Shule ya Sekondari Iguguno.

“Matumizi ya Wakandarasi yabaki katika miradi mikubwa tu lakini miradi yote midogo tuwatumie mafundi waliopo katika maeneo yetu, mafundi hawa wazawa wanatekeleza kazi kwa ubora kama huu ambao nimeuona leo na kwa gharama ambazo ni nzuri,” amesisitiza mara baada ya kutoa agizo hilo.

Maonyesho ya Utalii wa Tanzania Saudi Arabia yalivyofana

Maonyesho ya Utalii wa Tanzania yalivyofanyika mjini Riyadh nchini Saudi Arabia kwa watu mbalimbali kutembelea kwenye maonyesho hayo yaliyoandaliwa na Ubalozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia. Aidha Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia, H.E Hemed Mgaza yupo nchini Tanzania kwa ajili ya kupanda Mlima Kilimanjaro.
 Maonyesho yakiendelea kwa wageni mbalimbali kuelezewa namna ya vivutio vya utalii wa Tanzania.Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia, H.E Hemed Mgaza kushoto akiwa na mke wake, Maimuna Mgaza, wakiwa kwenye maonyesho hayo ya Utalii.

Monday, October 09, 2017

Mkuu wa Mkoa wa Singida aagiza kuvunjwa kwa Bodi ya Ushirika Iramba

 Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi akiwaelekeza wakulima wa pamba kijiji cha Msai wilayani Iramba, vipimo vya kati ya tuta na tuta, shimo na shimo kwa kutumia kamba na vijiti ili waweze kupanda kitaalamu na kuvuna kwa wingi.
 Wakulima wa pamba kijiji cha Msai wilayani Iramba, wakishiriki kwa vitendo mafunzo yya kupima urefu kati ya tuta na tuta, shimo na shimo kwa kutumia kamba na vijiti ili waweze kupanda kitaalamu na kuvuna kwa wingi.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi amemuagiza Mkuu wa Wilaya ya Iramba Emmanuel Luhahula, asimamie kuvunjwa kwa bodi ya Ushirika wa Kijiji cha Msai Wilayani Iramba ndani ya wiki mbili, kutokana na tuhuma za ubadhirifu wa zaidi ya shilingi milioni 50.

Dkt Nchimbi ametoa agizo hilo mwishoni mwa wiki alipokuwa katika mkutano na wakulima wa Pamba wa Kijiji cha Msai, ambao wamemueleza kutokuwa na imani na viongozi wa bodi hiyo kutokana na upotevu wa fedha hizo na wakiwa hawajachukuliwa hatua yoyote.

Wakulima hao wamemueleza Mkuu wa Mkoa kuwa fedha zaidi ya milioni 50 zilitolewa na seikali kwa ajili ya ujenzi wa Jengo la ghala la ushirika wa kijijini hapo lakini hakukuwa na ujenzi wowote uliofanyika huku wakifuatilia hawapewi majibu sahihi.

Madaktari Bingwa 18 wa Saudi Arabia kutua Zanzibar


Katika picha ni viongozi wa Madaktari wakiwa na Balozi Hemedi Mgaza na Afisa wa Ubalozi Bw. Ahmada Sufiani walipofika Ubalozi mjini Riyadh kujitambulisha.
 
Na Mwandishi Maalumu, Riyadh- Saudi Arabia

Kundi la madaktari bingwa 18 wa hiyari kutoka nchini Saudi Arabia linatarajiwa kuwasili tarehe 12 Oktoba ambapo wataweka kambi ya tiba (medical camp) kwa muda wa majuma miwili. Madaktari hao wanatarajiwa kufanya matibabu na upasuaji katika hospitali za kisiwa cha Pemba.


Akizungumza katika Ofisi za Ubalozi wa Tanzania mjini Riyadh wakati wa hafla ya kuagana na madaktari hao, Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia, Hemedi Mgaza, alisema kambi tiba hii ni ya pili kufanyika Zanzibar. Mwezi Novemba mwaka 2016 madaktari hao walifika Zanzibar na kuweka kambi ya kwanza katika kisiwa cha Pemba kwa mara ya kwanza kwa mafanikio makubwa.


Mwaka jana madaktari hao walipata ushirikiano wa kutosha kutoka kwa viongozi wa Wizara ya Afya ya Zanzibar na madaktari wenyeji, ndio maana wamependelea kurejea tena mwaka huu.


Pamoja na kutoa huduma za matibabu, madaktari hao watakwenda na dawa na vifaa tiba vya aina mbalimbali ambavyo Mwisho wa kambi watavitoa kama msaada kwenye hospitali hizo.

Tuesday, August 22, 2017

Serikali yaipa somo TANESCO
Na Khalfan Said, Dar es Salaam
NAIBU Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani, pichani anayeongea amelitaka Shirika la Umeme Tanzania TANESCO kuunganisha nguvu ili kuhakikisha wanakamilisha mradi wa ujenzi wa kituo cha kupoza na kusamabaza umeme kinachotarajiwa kujengwa huko Kimbiji wilayani Kigamboni jijini Dar es Salaam.
Dkt. Kalemani ametoa maelekezo hayo leo Agosti 22, 2017, wakati alipofanya ziara kukagua miradi ya umeme kwenye kituo cha kupoza na kusambaza umeme cha Kurasini, Kigamboni na eneo panapotarajiwa kujengwa kituo kingine cha kupoza na kusambaza umeme huko Kimbiji wilayani Kigamboni jijini Dar es Salaam.
“Hakikisheni mradi wa uejenzi wa kituo hiki cha Kimbiji unakamilika ifikapo Machi 30, mwakani,(2018), na kuwaondolea adha ya upatikanaji wa umeme wananchi wa Kigamboni, chukueni mafundi waliokamilisha kazi ya kujenga kituo cha umeme kule Mtwara waje hapa, muwaache wale wanaojenga transition (njia ya kusafirisha umeme) wajenge, lakini wale mafundi wengine waleteni hapa ili mradi huu ukamilike.” Alifafanua.

Mbunge wa Jimbo la Tunguu ashiriki kujenga madarasa saba

Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu Zanzibar Mhe Simai Mohammed Said akiwa na Wananchi wa jimbo lake katika Kisiwa cha uzi ngambwa wakishangilia wakati wa ujenzi wa Taifa wa kujenga madarasa saba ya Skuli ya Msingi  katika Kijiji cha Ngambwa kutowa elimu kwa watoto wa kijiji hicho kupata elimu ya msingi karibu na makaazi yao. Madarasa hayo yanajengwa kwa nguvu za Mwakilishi na Mbunge kwa Wananchi wa Jimbo lao.
Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu Zanzibar Mhe Simai Mohammed Said akizungumza na wananchi wa Kisiwa cha Uzi Ngambwa wakati wa ujenzi wa madarasa ya Skuli ya Msingi Ngambwa Uzi inayojengwa na Mbunge na Mwakilishi na nguvu Wananchi wa kijiji hicho. 

Mahujaji wa Tanzania 977 kati ya 2700 watua Saudi Arabia kwa ajili ya Ibada ya Hijja


Na Mwandishi Maalum Riyadh, Saudi Arabia
Mahujaji kutoka Tanzania wameanza kuwasili nchini Saudi Arabia kwa ajili ya kutekeleza nguzo ya tano ya dini ya kiislamu ya kuhiji Makkah inayofanywa na watu mbalimbali duniani, wakiwamo Waislamu kutoka Tanzania.
Baadhi ya mahujaji wakionekana Uwanja wa Ndege baada ya kuwasili nchini Saudi Arabia kwa ajili ya swala ya Hija.
 Mahujaji kutoka Tanzania wakiwa wamewasili nchini Saudi Arabia.

‘Tigo Fiesta 2017 – Tumekusoma’ kurindima katika mikoa 15 nchini

 Kaimu Meneja wa Masoko Tigo, William Mpinga(katikati) akizungumza na waandishi wa habari(hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa msimu mpya wa Tigo Fiesta 2017 'Tumekusomaa' leo jijini Dar es salaam. Kushoto ni Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi Tigo Fiesta, Sebastian Maganga na mwakilishi toka Basata, Mrisho Mrisho.
 Kaimu Meneja wa Masoko Tigo, William Mpinga(katikati) akizungumza na waandishi wa habari(hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa msimu mpya wa Tigo Fiesta 2017 'Tumekusomaa' leo jijini Dar es salaam. Kushoto ni Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi Tigo Fiesta, Sebastian Maganga na mwakilishi toka Basata, Mrisho Mrisho.
Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi Tigo Fiesta 2017, Sebastian Maganga (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari(hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa msimu mpya wa Tigo Fiesta 'Tumekusomaa' leo jijini Dar es salaam. Kushoto kwake ni Kaimu Meneja wa Masoko Tigo, William Mpinga na mwakilishi toka Basata, Mrisho Mrisho.

Mohamed Kivugo: Milioni 20 za Biko nitajengea nyumba


Mratibu wa Matukio na Mawasiliano wa Biko, Hassan Melles kulia mwenye fulana ya Biko akimkabidhi fedha zake mshindi wao wa Bahati Nasibu, Mohamed Kivugo aliyeibuka kidedea katika droo ya 33 iliyochezeshwa Jumapili. Kushoto ni Afisa wa NMB, Tawi la Bank House, Posta jijini Dar es Salaam akishuhudia makabidhiano hayo.

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
FUNDI magari mkazi wa Tabata, jijini Dar es Salaam, Mohamed Kivugo mwenye miaka 45, amesema kwamba fedha zake alizokabidhiwa jana baada ya kushinda kwenye Bahati Nasibu ya Biko 'Ijue Nguvu ya Buku', atazitumia kujengea nyumba ili aondokane na changamoto ya makazi.

Kivugo aliyasema hayo jana wakati anapokea zawadi ya Sh Milioni 20 za ushindi wa Biko alizokabidhiwa katika benki ya NMB,  tawi la Bank House Posta, jijini Dar es Salaam.

Mshindi wa Sh Milioni 20 wa Bahati Nasibu ya Biko, Mohamed Kivugo akiwa ameshika fedha zake baada ya kukabidhiwa jana katika Tawi la NMB la Bank House, Posta, jijini Dar es Salaam tayari kwa matumizi yake ya kawaida.

Akizungumza katika makabidhiano hayo, Kivugo alisema dhamira yake kubwa ni kutatua changamoto ya makazi kwa kuzitumia fedha za Biko kujenga nyumba. 

"Ingawa nimepata ushauri mzuri kutoka kwa watu wa NMB baada ya kukabidhiwa fedha zangu kutoka Biko baada ya kushinda kwenye droo ya 33 iliyochezeshwa Jumapili, lakini naamini wazo la nyumba ni zuri kwangu.

Tuesday, August 15, 2017

Irene Kitinga: Ukitaka kujua Nguvu ya Buku ya Biko uibuke na ushindiNa Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
MSHINDI wa Sh Milioni 20 za Bahati Nasibu ya Biko ‘Ijue Nguvu ya Buku’, Irene Kitinga, amepokea fedha zake katika benki ya NMB, Tawi la Bank House jijini Dar es Salaam, huku akisema kuwa ukitaka kujua nguvu ya mchezo huo uibuke na ushindi.
Mratibu wa Matukio na Mawasiliano wa Biko Tanzania, Hassan Melles, akimkabidhi jumla ya Sh Milioni 20 mshindi wao wa Ubungo, jijini Dar es Salaam, Irene Kitinga, katika benki ya NMB jana Jumatatu. Kushoto ni Afisa wa NMB Tawi la Bank House Posta, jijini Dar es Salaam akishuhudia makabidhiano hayo.
 

Irene mkazi wa Ubungo, jijini Dar es Salaam, alikabidhiwa fedha  zake juzi na  Mratibu wa Matukio na Mawasiliano wa Biko, Hassan Melles, ikiwa ni siku moja tu tangu atangazwe mshindi kwenye droo ya 31 iliyochezeshwa jana.

Akizungumza katika makabidhiano hayo, Irene alisema kwamba wengi hawaaamini kwamba fedha hizo hazitoki, jambo ambalo huthibitishwa sio kweli mtu anapofanikiwa kuibuka na ushindi wa zawadi za Biko zinatoka kuanzia Sh 5,000, 10,000, 20,000, 50,000, 100,000, 500,000 na Sh Milioni moja, bila kusahau donge nono la Sh Milioni 20 linalotoka kila Jumatano na Jumapili.

Mshindi wa Sh Milioni 20 wa Bahati Nasibu ya Biko droo ya 31, Irene Kitinga, akipokea fedha zake kutoka kwa Mratibu wa Matukio na Mawasiliano wa Biko Tanzania, Hassan Melles kulia katika benki ya NMB Juzi Jumatatu.
 

Alisema hata yeye pia alidhani ni utani alipokuwa anapokea simu ya Kajala Masanja, hivyo ni wakati wa kila mtu kucheza Biko ili ajiwekee mazingira mazuri ya ushindi kama sehemu ya kutafuta fursa za kiuchumi kwa kutumia mchezo wa Biko.

TFF yamlilia marehemu Dyamwale aliyekuwa Mbunge wa zamani wa Handeni

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
WAKATI marehemu Hassan Chabanga Dyamwale mbunge wa zamani wa Handeni, mkoani Tanga, akitarajiwa kusafirishwa leo kuelekea nyumbani kwao Handeni tayari kwa maziko, Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Wallace Karia ametuma salamu za rambirambi kufuatia kifo cha aliyewahi kuwa Katibu Mtendaji wa kilichokuwa Chama cha Mpira wa Miguu Tanzania (FAT), Chabanga Hassan Dyamwale (76).

Mbali wa wadhifa huo katika eneo la mpira wa miguu,  pia Dyamwale atakumbukwa zaidi akiwa Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii na kwa miaka ya hivi karibu alikuwa Mjumbe wa Kamati huru ya uchaguzi TFF tangu 2004 mpaka 2012.

Hayati Dyamwale aliyezaliwa Juni 01, 1941, aliondoka FAT mwaka 1978, lakini pia aliwahi kuwa Mkurugenzi wa Michezo nchini miaka ya mwanzo ya 1980 kabla ya kuhamishiwa Handeni mkoani Tanga kuwa Ofisa Utamaduni, lakini Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati huo, Mwalimu Julius Nyerere akamrudisha Dar es Salaam.

“Nimeguswa na kifo cha Mzee Chabanga Hassan Dyamwale. Inna Lillah wainaillah Rajauun. Natuma salamu zangu za rambirambi kwa familia, ndugu, jamaa, majirani na marafiki wa hayati Mzee Dyamwale ambaye nimetaarifiwa kuwa amefariki dunia Agosti 13, mwaka huu kwenye Hospitali ya Muhimbili,” amesema Karia.

“Ni msiba mkubwa kwa wanafamilia ya michezo hususani soka,” amesisitiza Rais Karia na kuomba  familia, ndugu, jamaa, marafiki kuwa watulivu katika kipindi hiki kigumu baada ya kumpoteza mpendwa Dyamwale.

Rais Karia amesema: “Namfahamu Mzee wetu huyu tangu miaka mingi akiwa mteuliwa kutoka serikalini kushika wadhifa wa utendaji ndani ya FAT wakati ule (Kwa sasa ni TFF), alifanya kazi kwa uhodari mkubwa na uadilifu,” amesema Rais Karia.

Rais Karia amesema kwamba mbali ya kuwa mtendaji ambaye alifanya mabadiliko makubwa katika soka la Tanzania kutoka ligi ya kituo kimoja hadi ligi ya mikondo miwili (nyumbani na ugenini). Taarifa zinasema kwamba alifanya kazi hiyo akiwa kwenye hema.

Pia Rais Karia alimfahamu Mzee Dyamwale alipokuwa Meneja wa Uwanja wa Taifa (sasa Uwanja wa Uhuru) aliyekuwa mtaalamu wa masuala ya ujenzi wa viwanja.

Rais Karia amesema kwamba atambukuka zaidi hayati Dyamwale kwa uhodari wake wa kazi na msimamo kwenye jambo aliloliamini lilileta mafanikio makubwa katika soka la Tanzania.

Kumbukumbu nyingine zinaonesha kuwa Dyamwale ndiye aliyebuni mpango wa watoto kuingia bure uwanjani miaka ya 1980 maarufu yosso. Marehemu Dyamwale anatarajiwa kusafirishwa leo kuelekea wilayani Handeni, mkoani Tanga kwa ajili ya maziko yatakayofanyika huko nyumbani kwao Handeni.

Friday, August 11, 2017

Mshindi wa Milioni 20 za Biko Kimara Suka akabidhiwa fedha zake

Mshindi wa Biko droo ya 30, Anthony Chitanda, akionyesha shangwe zake baada ya kupokea fedha zake Sh Milioni 20 kutoka Biko kama sehemu ya ushindi wake.


Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
MSHINDI wa Shilingi Milioni 20 za Biko kutoka kwenye Bahati Nasibu ya Biko ‘Ijue Nguvu ya Buku’, Anthony Chitanda, amekabidhiwa fedha zake mapema jana katika benki ya NMB, Tawi la Bank House, Posta, jijini Dar es Salam, sambamba na kupewa ushauri wa kifedha.

Chitanda aliibuka kidedea katika droo ya 30 ya Biko iliyochezeshwa juzi Jumatano na kuvuna Sh Milioni 20 zinazotolewa na waendeshaji hao wa Biko, mchezo wa kubahatisha unaoendelea kutingisha katika wilaya na mikoa mbalimbali ya Tanzania.
Mratibu wa Matukio na Mawasiliano wa Bahati Nasibu ya Biko, Hassan Melles kulia amkabidhi mshindi wao wa droo ya 30 Anthony Chitanda katikati katika benki ya NMB, Tawi la Bank House, Posta, jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Afisa wa NMB. Makabidhiano hayo yalifanyika jana mchana.

Akizungumza katika Makabidhiano hayo, Mratibu wa Matukio na Mawasiliano wa Biko, Hassan Melles, alisema kwa kila anayecheza bahati nasibu yao, lazima ajiandae kulala masikini na kuamka tajiri.


Alisema ushindi wa Biko ni rahisi kwa wale wanaocheza kwa kutumia mitandao ya simu ya M-Pesa, Tigo Pesa na Airtel Money ambapo namba ya Kampuni ni 505050 na kumbukumbu ni 2456, huku kianzio cha kuchezea Biko kikianzia Sh 1,000 na kuendelea.

Tuesday, August 08, 2017

Innocent Nyeriga: Milioni 20 za Biko nitajengea nyumba

Mshindi wa Droo ya 29 ya Biko, Innocent Nyeriga wa pili kutoka kulia akipokea fedha zake kutoka kwa Mratibu wa Matukio na Mawasiliano wa Biko, Hassan Melles wa pili kutoka kushoto mwenye fulana ya Biko.


Na Mwandishi Wetu, Dodoma
KUTOKANA na changamoto nyingi za ukosefu wa makazi ya kuaminika kwa watu wengi, mshindi wa Sh Milioni 20, Innocent Nyeriga, amesema anatafakari fedha zake alizokabidhiwa jana mjini Dodoma aziweke kwenye ujenzi wa nyumba.

Nyeriga mkazi wa Dodoma na mshindi wa Biko droo ya 29 iliyochezeshwa mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam, alikabidhiwa fedha zake jana Jumatatu katika benki ya NMB, Mjini Dodoma tayari kwa kuanza kuzitumia kwa matumizi yake ya kawaida.

Akizungumza kwa furaha kubwa, Nyeriga anayejighulisha na kibarua cha kuhudumia mifugo mjini Dodoma, alisema kwamba lengo lake haswa ni kujenga nyumba nzuri ili familia yake iondokane na changamoto ya ukosefu wa makazi bora.
Shughuli ya makabidhiano ya Sh Milioni 20 kwa mshindi wa Dodoma, Innocent Nyeriga ikiendelea katika benki ya NMB jana mjini Dodoma.

Sunday, August 06, 2017

Innocent Nyalia wa Dodoma achomoza na Milioni 20 za Biko

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
MKAZI wa Dodoma nchini Tanzania, Innocent Nyalia, ameibuka na ushindi mnono wa Sh Milioni 20 kutoka kwa waendeshaji wa Bahati Nasibu ya Biko ‘Ijue Nguvu ya Buku’, katika droo iliyochezeshwa leo jijini Dar es Salaam.
Droo hiyo ilichezeshwa na Balozi wa Biko, Kajala Masanja na Mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Jehud Ngolo, ambaye kwa pamoja alishuhudia kupatikana kwa mshindi huyo wa droo ya 29 ya Biko.

Akizungumza katika droo hiyo, Mratibu wa Masoko na Mawasiliano wa Biko, Hassan Melles, alimpongeza mshindi huyo wa mjini Dodoma, Nyalia na kuwataka Watanzania wote kuchangamkia fursa za mamilioni ya Biko.

Alisema huu ni wakati wa kutajirika kwa kuvuna mamilioni ya Biko yanayoendelea kutolewa kwa wingi, ikiwa ni mwendelezo wa kuona wachezaji hao wanaotumia simu za M-Pesa, Airtel Money na Tigo Pesa kwa kuingiza namba ya kampuni 505050 na kumbukumbu 2456 wananeemeka na Biko.

“Kama kawaida yetu ushindi wa Biko ni rahisi kupatikana na kucheza kwake kuliko michezo mingine yoyote, hivyo tunawaomba Watanzania wasilaze damu katika mchezo wetu wa Biko unaozidi kutoa mamilioni ya fedha.

Thursday, August 03, 2017

Moses Matagili akabidhiwa Milioni 20 zake


Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

WAENDESHAJI wa bahati nasibu ya Biko ‘Ijue Nguvu ya Buku’, leo wamemkabidhi jumla ya Sh Milioni 20, mshindi wao wa droo ya 28, Moses Matagili, mkazi wa Goba, aliyetangazwa jana Jumatano, jijini Dar es Salaam.
Moses Matagili mshindi wa Biko wa Milioni 20 mkazi wa Goba, katikati akipokea fedha zake kutoka kwa Mratibu wa Matukio na Mawasiliano wa Biko, Hassan Melles kulia, huku akishuhudiwa na afisa wa NMB, tawi na Bank House, jijini Dar es Salaam leo mchana.
 

Matagili anakuwa mshindi wa droo ya 28 ya Biko, inayochezwa kwa njia ya ujumbe mfupi wa maandishi kwa kufanya miamala kwenye simu za M-Pesa, Tigo Pesa na Airtel Money kuanzia Sh 1,000 na kuendelea, huku namba ya kampuni ikiwa ni 505050 na kumbukumbu ni 2456.


Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa fedha zake, Matagili anayejishughulisha na kazi za ujenzi wa nyumba, alisema amepokea ushindi wake kwa furaha, baada ya kuuwazia kwa muda mrefu na kuamua kuwa mchezaji mzuri wa Biko.
Mshindi wa droo ya 28 ya Biko, Moses Matagili, kushoto akipokea fedha zake jumla ya Shilingi Milioni 20 kutoka kwa Mratibu wa Matukio na Mawasiliano wa Biko, Hassan Melles kulia katika benki ya NMB leo jijini Dar es Salaam.

Wednesday, August 02, 2017

WFP yatambulisha mikakati ya kutokomeza njaa nchini

 Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Chakula Duniani (WFP) Bw. Michael Dunford akielezea kwa undani namna shirika hilo litakavyoweza kufanya kazi nchini Tanzania na kuitaja mikakati mitano waliyo iweka kwa ajili ya Shirika hilo.
 Mmoja wa Blogger Bw. Bethuel Kinyori ambaye ni Mmiliki wa mtandao wa Dailypulse24.com akiuliza swali wakati wa Mkutano huo ulio fanyika katika Hotel ya New Africa Jijini Dar es salaam leo.
 Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Chakula Duniani (WFP) Bw. Michael Dunford akijibu baadhi ya maswali yaliyoulizwa na waandishi wa Habari za Mtandaoni.

Milioni 20 za Biko zamfikia Moses Matagili wa GobaNa Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
BAHATI Nasibu ya Biko ‘Ijue Nguvu ya Buku’, droo ya 28 imefanyika leo, huku mkazi wa Goba, jijini Dar es Salaam, Moses Matagili, akifanikiwa kuibuka kidedea kwa kushinda Sh Milioni 20.
 Kajala Masanja Balozi wa Biko Tanzania.
Droo hiyo iliyofanyika jana, ilichezeshwa na Balozi wa Biko, Kajala Masanja kwa kushirikiana na mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Jehud Ngolo.

Akizungumza baada ya kumpata mshindi huyo, Mratibu wa Matukio na Mawasiliano wa Biko, Hassan Melles, alisema sasa ni wakati wa kuchangamkia fursa ya kuibuka na mamilioni kwa kucheza Biko inayotoa ushindi wenye fursa ya kiuchumi.

Alisema kwamba droo kubwa ya kuwania Sh Milioni 20 inafanyika Jumatano na Jumapili, huku Jumatano hii ikienda kwa Matagili, ambaye ni mkazi wa Goba, sanjari na washiriki kuvuna zawadi mbalimbali za fedha taslimu kuanzia Sh 5,000, 10,000, 20,000, 50,000, 100,000, 500,000 na Sh Milioni moja.

“Tunampongeza mshindi wetu wa droo ya 28, Matagili kwa kuvuna donge nono la Sh Milioni 20 kutoka Biko, hivyo tunawaomba Watanzania wengine waendelee kucheza Biko ili waweze kujipatia zawadi mbalimbali kutoka kwetu.

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...