https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543


Recent Post

Wednesday, December 19, 2012

Bahati Bukuku: Wahindi ndio wezi wakubwa




Mwimbaji Bahati Bukuku akizungumza na Handeni Kwetu akiwa na uchungu mkubwa. Angalia mwenyewe uso wake. Duh.
 
Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
MWIMBAJI wa muziki wa Injili hapa nchini, Bahati Bukuku, amesema Wahindi wanaojihisisha na uuzaji wa kazi za wasanii Tanzania ndio wezi wa kutupwa, hivyo hawastahili kuruma.

Bukuku aliyasema hayo muda mchache uliopita alipokuwa akizungumzia masuala ya wasanii na maendeleo yao, Sinza, jijini Dar es Salaam, ikiwa ni juhudi za kujikomboa kimaisha.

Msanii huyo anayeng’ara katika 'game' na wimbo wake wa 'Dunia Haina Huruma', alisema kama wapo wadau wanaotaka Wahindi wapewe suala la kudhibiti wizi huo basi wanajidanganya.

Alisema hata suala la stika inayobandikwa kwenye CD ya msanii haiwezi kuwanufaisha wasanii kama jukumu hilo litaachwa kwa wafanyabiahara wenyewe badala ya serikali.

“Huu ni utumbo na haiwezi kukubalika suala la wizi wa kazi za wasanii kuachwa kwa wafanyabiashara wenyewe wakiwamo Wahindi ambao hao ndio wabaya wetu.

“Jamani jambo hili litaendelea kutumbua na sisi wasanii tusikubali jambo hili kufanywa kisiasa badala ya kuwakombao wasanii wanaoendelea kunufaisha matajiri wenye roho mbaya,” alisema Bukuku.

Bukuku katika mazungumzo hayo, aliitaka serikali kujiingiza kwa dhati katika mapambano hayo, huku akitoa ushauri stika zinazobandikwa zitofautiane kwa kila msanii.

Leo waimbaji wa Injili wameandaliwa kikao cha pamoja katika Hoteli ya Wanyama iliyopo Sinza Mori, jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuangalia changamoto zao, wakiwa chini ya Mfuko wa Pensheni wa LAPF.
 


No comments:

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...