Raha
za mwenzi wako zipo kwenye himaya yako wewe
Na Kambi
Mbwana
MAPENZI ni jambo ambalo linaleta hisia mbili
tofauti. Mosi; mapenzi yanaweza kukufanya uishi kwa raha kama mfalme. Pili,
mapenzi hayo yakibadilika hukufanya uwe kama chizi.
Jambo hilo zuri linalofananishwa na sukari kwa
yaliyowakalia vizuri, hubadilika na kuwafanya baadhi yao waone ugumu wa
kuendelea kuishi, maana wanaowapenda wanawasumbua kwa kiasi kikubwa.
Ni kutokana na hilo, jamii inashauriwa kuwa
makini katika suala hilo. Wasijaribu kukurupuka na kuchukua uamuzi wenye mashaka
kwa namna moja ama nyingine, maana vinginevyo watatamani kujinyonga.
Hata hivyo, pamoja na yote hayo, lakini
inajulikana wazi wazi kuwa dawa kubwa katika uhusiano wa kimapenzi ni kumfikisha
mwenzako, kumuweka katika kilele cha ubora katika ulimwengu wa mapenzi.
Katu usiangalie umbo lako, sura yako katika
kujigamba kwamba unaweza kupendwa na yoyote, wakati ni mzigo kitandani. Kama
huna ujuzi katika suala la mapenzi, ondoa kupendwa, kuhitajiwa au kugandwa na
yoyote.
Zaidi ya hapo, wachache wao watakupitia na
kuchukua hamsini zao, maana huna ujanja wa kumuweka mwenzako katika furaha.
Hivyo basi, ili jamii iwe kwenye ramani nzuri na furaha ya mapenzi, lazima
tuwajulie watu wetu.
Tufahamu namna ya kuwachanganya kisaikolojia,
bila kuangalia uzuri wetu, fedha zetu, maana hizo haziwezi kufanya penzi liwe na
amani.
Wapo ambao wanaishi na wanaume wenye nazo
kupita kiasi, lakini bado wake zao, wachumba zao au wapenzi wao wanajiingiza
katika uhusiano na watu wa kawaida, wakiwamo wafanyakazi wa ndani.
Hata hivyo haitoshi, wapo pia wakina mama wenye
nazo lakini wanachanganywa na wasichana wa kawaida, wenye sura za kawaida au
hadhi za kawaida. Wenye mali zao wanalia na kusaga meno.
Wanasema“Hivi kwani mume wangu unatembea na
yule mfanyakazi wa ndani wakati mimi nipo” Au sielewi unachofuata kwa yule
kijana mchunga mbuzi wakati mimi nipo, tena mwenye fedha za kutosha tu”
Kama wewe ni miongoni mwa watu wenye mtazamo huo umeliwa. Fedha sio kila kitu katika mapenzi. Fedha zako usipoangalia zinaweza kuwanufaisha wapita njia, wajuzi wa mambo kwenye mambo fulani muhimu.
Huo ndio ukweli wa mambo. Mjuzi huyo hatafutwi
ili mradi mtu ana mtu wa nje, ila umuhimu wake unakuja anapokuwa kwenye ulingo.
Hayo lazima mimi na wewe tuyajuwe kwa ajili ya mapenzi yetu.
Unapokuwa na mpenzi wako, mume au mke wako
lazima ujuwe yupo na wewe kwa ajili ya kujenga maisha ya wawili. Ili mwenzako
afurahie uwepo wako, hakikisha kuwa walau unatumia muda wako hata kama kidogo
kumridisha kimapenzi.
Kwa wale ambao kwa miaka mingi wameishi na
wapenzi wao bila kutumia ujuzi wao, waanze leo. Na wale wanaoingia kwenye
uhusiano leo, pia wawaangalie watu wao, namna gani walivyo na wanastahili aina
gani ya mapenzi.
Ninaposema mapenzi, sio yale ya kukaa pamoja,
kutembea pamoja au kumpigia simu kila baada ya dakika kumi. Mapenzi, tendo la
ndoa lenye ujazo mkubwa linalostawisha uhusiano wa wawili wapendanao.
Hivyo basi tuwe makini katika kazi hiyo.
Tukitaka kuwapa raha kweli wenzetu lazima tuache kazi na kufanya kazi. Tendo la
ndoa sio mchezo mdogo. Sio kama kuwasha njiti ya kibiriti mahala
palipotulia.
Inahitaji kusumbua akili na kusumbua pia mwili
wako. Sina maana kama nataka muda wote muwe kwenye tendo la ndoa, ila mnapotaka
kufunja amri hiyo ya sita, basi mfikishe mwenzako kileleni.
Usimchezee chezee tu ukamuacha. Nimeamua
kuandika mada haya maana nimepata malalamiko mengi kutoka kwa wanawake. Baadhi
ya wasomaji wangu, wamenipasha kwamba waume zao ni watu wa kwenda raundi moja
halafu wanaangalia ukutani.
Kwa bahati mbaya, watu hao wanapolala uzungu wa nne, wanakuwa wanawanyanyasa wenzao, kama unavyojua tena gari linapowaka. Hali hiyo inakera kiasi cha kutamani wapiti njia.
Haya nayasema kwa uchungu, maana usaliti mwingi
huibuka kama wawili wapendanao hawaridhishani. Kama unaona huna ujuzi wa
kumuweka katika kilele mwenzako, tafuta msaada kwa watu.
Kabla ya kuendelea, niseme tu kutokana na aina
ya gazeti lako la Mtanzania, tunashindwa kuandika kiundani zaidi mada za
mapenzi, badala yake tunakuwa wepesi kujibu maswali yenu kwa kupitia simu au
barua pepe.
Tunafanya hivyo baada ya kugundua kwamba watoto
wengi nao hujifunza kinachoandikwa kwenye gazeti, jambo linalonifanya niandike
kwa kuficha au yale yasiyokuwa ya ndani zaidi.
Tukutane wiki ijayo.
0712 053949
0753 806087
No comments:
Post a Comment