Baadhi ya wanachama 698 waliotisha mkutano wa Simba, wakimsikiliza mwenyekiti wao wa muda, Dk Mohamedi Wande katikati aliyokaa karibu na Bi Hindu. Picha na Kambi Mbwana.
Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
BUNDI ametua tena katika
klabu ya Simba, baada ya wanachama wanaofikia 698 kuitisha Mkutano wa Dharura
uliopangwa kufanyika Travertine Hoteli, Desemba 30 mwaka huu, kwa ajili ya
kujadili mambo yanayohusu timu yao.
Mkutano huo unafanyika wakati
uongozi wa Simba, kupitia Mwenyekiti wao, Ismail Aden Rage kutangaza kuwa
wanaotangaza mkutano huo ni wahuni na hawawezi kumsumbua kwa njia yoyote.
Akizungumza mapema leo
mchana, Mwenyekiti wa muda wa walioitisha mkutano huo, Mohamed Wandi, alisema
kwamba wanachama wote wenye mapenzi mema na timu yao wanaombwa kufika kwa wingi.
Mwenyekiti wa Simba, Ismail Aden Rage
Alisema timu yao
inaendeshwa ovyo ovyo pamaja na kukanyagwa kwa Katiba yao iliyosababishwa wanaotaka mkutano huo
kuitwa wahuni na uongozi wa Simba.
Ibara ya 22 kifungu cha 2 cha
Simba SC
kinasema kuwa wanachama hai waliofikia 500 wanaweza kuitisha mkutano wa dharura
hasa kama Kamati ya Utendaji itashindwa kuitisha mkutano kama
inavyohitajiwa na wanachama hao.
“Hii haiwezi kukubalika hata
kidogo, maana mkutano wa dharura ni haki ya msingi kwa kila mwanachama ili
mradi wawe wametimia wanachama 500, hivyo tayari tumezidi maana sasa wapo watu
698 wanotaka mkutano huo.
“Uamuzi utakaotolewa utakuwa
wa haki na kusikilizwa na kila mtu, maana tayari uongozi hautaki kusikiliza
madai yetu, hasa walipotaka mkutano kwa ajili ya kujipanga na ligi mzunguuko wa
pili, usajili na namna gani ya kuiendeleza timu yetu na kuwa ya mfanao Barani Afrika,” alisema.
Kuitishwa upya kwa mkutano
huo huenda kukawa moto mpya kwa Rage, hasa kama
alijua wanachama hao wametulia, hasa walipokuwa wakisubiri siku zao 30
walizowapa uongozi kufikiria namna ya mkutano wao.
Katika hatua nyingine,
wanachama wanaopenda kuhudhuria mkutano huo wanapaswa kulipia kadi zao kwa wale
wanaodaiwa kutokukidhi vigezo vya kuwa wanachama, huku nakala za kuitisha
mkutano huo zikisambazwa Kwa Msajili wa Vyama vya Michezo na vila Tanzania, TFF
kwa kupitia Mwenyekiti wa Kamati ya Sheria na Katiba, DRFA, IDRFA na Kamanda wa
Polisi Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni.
No comments:
Post a Comment