Rais wa TFF, Leodgar Tenga
Na Kambi
Mbwana, Dar es Salaam
Waraka
wa marekebisho ya Katiba ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) umepita
baada ya kuungwa mkono na theluthi mbili ya wajumbe wa Mkutano Mkuu waliopiga
kura.
Ofisa
Habari Shirikisho hilo, Boniface Wambura, aliiambia Handeni Kwetu kuwa jumla ya
wajumbe waliopiga kura kwa njia hiyo ya waraka ni 103 ambapo 70 wameunga mkono
wakati waliokataa ni 33. Idadi hiyo ni asilimia 68 ya kura zote zilizopigwa,
hivyo kupatikana theluthi mbili ya kura zilizopigwa ili kufanya marekebisho
kikatiba.
Alisema
kura zilizosema ndiyo kutoka kwa wajumbe wa Mkutano Mkuu wa vyama vya mikoa ni
46, wajumbe kutoka vyama shiriki ni 13 wakati klabu za Ligi Kuu zilizounga
mkono ni kumi na moja.
Kamati
ya Utendaji ya TFF inawashukuru wajumbe wote wa Mkutano Mkuu- kwa waliounga
mkono na waliokataa kwa vile walikuwa wanatekeleza wajibu wao wa kikatiba.
Vipengele
vilivyoingizwa ni ‘club licencing’ kama ilivyoagizwa na Shirikisho la Mpira wa
Miguu Afrika (CAF), Kamati ya Rufani ya Uchaguzi wa TFF kama ilivyoshauriwa na
Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) na kuondoa nafasi ya Makamu wa
Pili wa Rais.
Vilevile
Kamati ya Utendaji itakutana Desemba 23 mwaka huu kufanya marekebisho ya Kanuni
za Uchaguzi, kutokana na kupitishwa kwa marekebisho hayo ambayo yanaunda Kamati
ya Rufani ya Uchaguzi wa TFF. Pia itachagua wajumbe wa Kamati ya Rufani ya TFF.
Mkutano
Mkuu wa TFF ambapo pia utakuwa na ajenda ya uchaguzi utafanyika Februari 23 na
24 mwakani. Kwa mujibu wa Katiba ya TFF, wajumbe wanatakiwa kupewa taarifa ya
Mkutano Mkuu siku 60 kabla.
No comments:
Post a Comment