Penina huyo katika pozi
Na Kambi
Mbwana, Dar es Salaam
MCHEZA
filamu za kibongo Tanzania, Jenifer Raymond, maarufu kama Penina, amesema baada
ya kubadili dini na kuwa Muislamu, ametulia na kuangalia zaidi maisha yake ya
ndoa aliyofunga na mwarabu mmoja jina lake linahifadhiwa kwa sababu maalumu.
Penina akiwa na msanii mwenzake Mshindo Jumanne
Penina
aliyewika zaidi katika sanaa, alitangaza kubadili dini hiyo kwasababu ya kutaka
ndoa ya mwarabu mmoja.
Akizungumza
na Handeni Kwetu mapema leo, Penina alisema aliamua kubadili dini kwa ridhaa
yake akiwa na lengo la kuacha usichana wake.
Alisema katika maisha yake ya ndoa na mume wake huyo, ameweza kuvaa vyema uhusika wake, ingawa soko la sanaa bado analitendea, huku akiongeza kuwa u siri wa ndoa yao unatokana na kuogopa media zinavyoweza kuingilia kati na kuvuruga mapenzi ya watu.
Penina kama kawaida yake
“Nimeamua
mwenyewe kubadili dini na kuolewa na mwarabu nikifuata dini yake ya Uislamu,
lakini siri ilikubwa kubwa kwasababu bila hivyo ndoa yetu inaweza kuvunjika
hasa kama wote tutakuwa wepesi kusoma na kuvifanyia kazi vichwa vya habari.
Penina
alicheza filamu nyingi ikiwamo hiyo ya Penina aliyocheza na marahemu Steven
Kanumba, Dar es Salaam na nyinginezo nyingi zilizompa umaarufu hapa nchini.
No comments:
Post a Comment