Na Kambi
Mbwana, Dar es Salaam
BENDI ya
FM Academia, maarufu kama ‘Wazee wa Ngwasuma’, leo Desemba 25 wanatarajia kutoa
burudani katika Ukumbi wa Arcade Hose, Mikocheni kwa ajili ya kuwapa raha
mashabiki wao katika Sikukuu ya Krismasi.
Shoo hiyo
itakuwa ya aina yake, huku ikiporomoshwa na magwiji wa muziki wa dansi nchini,
akiwamo Patchou Mwamba, Nyosh El Sadaat na wengineo wenye lengo la kuonyesha
uwezo wao.
Akizungumza
mapema leo asubuhi, Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa bendi hiyo, Kelvin
Mkinga, alisema kwamba maandalizi ya maangamizi ya burudani hiyo yamekamilika.
Alisema
wanamuziki wake wote wote wapo kwenye uwezo wa juu kwa ajili ya kuwapatia raha
mashabiki wao katika Ukumbi huo wa kisasa.
“Huu ni
wakati wa kufanya mapinduzi katika tasnia ya muziki wa dansi hapa nchini, hivyo
naomba wadau na mashabiki wetu waje kwa wingi Arcade siku ya Krismasi.
“Nyimbo
zetu zinazopendwa na mashabiki wetu zitaimbwa, huku tukiamini kuwa tunashiriki
kwa dhati kufurahia na kumuomba Mungu tuumalize mwaka salama,” alisema Mkinga.
Baadhi ya
nyimbo zinazopendwa na watu wengi ni pamoja na Heshima kwa Mwanamke, Anna, Vuta
Nikuvute, Otilia na nyinginezo zinazofanya vyema kutokana na kuimbwa kwa ufundi
wa aina yake.
No comments:
Post a Comment