Na Rahimu Kambi, Handeni
MKUU wa
wilaya ya Handeni, Muhingo Rweyemamu, amewataka watu kuacha kupanga mkaa
barabarani ili waweze kuilinda barabara hiyo inayotoka Mkata kwenda Handeni.
Muhingo
aliyesema hayo hivi karibuni aliposhuka kwa ajili ya kuwaelimisha wananchi hao
wanaofanya biashara hiyo inayoweza kuhatarisha usalama wa barabara hiyo.
Akizungumza
na Handeni Kwetu, alisema ingawa juu ya biashara ya mkaa ipo chini ya Wizara ya
Maliasili na Utalii, lakini ofisi yake inaingilia kati kwa kuwataka watu hao
kuacha kupanga bidhaa zao barabarani.
Alisema
yeye kama Mkuu wa wilaya ya Handeni anazuia kupanga mkaa, maana unaongoza
kuharibu kuta za barabara hiyo iliyojengwa kwa ajili ya kuharakisha maendeleo yao.
“Nawaomba
jamani mnapokuwa kwenye biashara hii hakikisheni bidhaa zenu hazipo barabarani
kwa ajili ya kuilinda barabara hii nzuri kwa ajili yetu.
“Tusipokuwa
makini, barabara itaharibika mapema wakati hata kukabidhiwa bado, hivyo naomba
tuelewane katika hili, japo najua mpo kimakosa mnapofanya biashara hii ya
mkaa,” alisema Muhingo.
Kujengwa
kwa barabara ya Mkata Handeni kumepokelewa kwa furaha na wakazi wengi wa
Handeni, hasa wa maeneo korofi ya Kwachaga ambayo mvua inaponyesha kidogo tu,
magari hukwama na kushindwa kuendelea na safari zake.
No comments:
Post a Comment