HII ni
mara ya tatu kuandaa TOTO PARTY kwa ajili ya watoto wa jiji la Dar es Salaam na
itafanyika Krismasi na Boxing Day ndani ya Cine Club.
Katika
Tamasha hilo, watoto watapata nafasi ya kushiriki
katika michezo mbalimbali kama soka la
ufukweni, kuogelea, kusaka hazina (Treasure hunt) na kujipaka rangi usoni (Face
painting) na mengine mengi.
Aidha
watoto hao pia wataweza kufunga akaunti ya benki kwa watoto inayojulikana kama ‘Pambazuka’ kupitia benki ya Ecobank.
Mbali na
watoto kucheza na kufurahi michezo mbalimbali pia wazazi wao watachuana katika
mchezo wa kuvuta kamba ambapo washindi katika michezo hiyo watazawadiwa zawadi
mbalimbali na viingilio ni Sh 3,000 kwa watoto na wakubwa Sh 7,000.
No comments:
Post a Comment