GAZETI
la Mtazania Jumapili la Desemba 16 lilichambua kwa kina makala iliyokwenda kwa
jina la Sera ya Umeme vijijini ipo kwenye makaratasi.
Kambi Mbwana, mwandishi wa maoni haya
Baada
ya kutoa makala hiyo ambayo ni kolamu inayotoka katika gazeti hilo kila
Jumapili, pia iliingia kwenye blog yangu kama
utaratibu wangu.
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo
Nasikitika
kuona Serikali kwa kupitia Wizara ya Nishati na Madini chini ya Wakala wa
Nishati Vijijini (REA) wakaanza kujibu kwa mtindo wa tangazo katika magazeti
hapa nchini na kutumia fedha vibaya.
Ifikie
wakati tuwe na huruma na fedha za Serikali. Wakala wa Nishati Vijijini (REA),
wanatumia gharama kubwa kujisafisha kwasababu ya makala yangu moja tu iliyosema
Sera ya Umeme vijijini ipo kwenye makaratasi.
Gazeti
la leo la Raia Mwema wametoa matangazo full page 2 kama
ilivyokuwa kwa Mwananchi jana.
Hadi
sasa ni dhahiri wametumia fedha zisizozidi Milioni 10 na sijui wataacha lini kutoa
matangazo. Jana walikuwa Mwananchi, leo wamepewa Raia Mwema.
Ila najua bado magazeti mengine yenye nguvu, kama
vile Tanzania Daima, Majira, Nipashe na Gazeti la Serikalai Habari leo.
Mbaya
zaidi wanatoa matangazo mahali ambapo makala hiyo haijaandikwa wala haijasomwa?
Kwanini? Huu ni utendaji kazi gani usiokuwa na huruma na Taifa letu? Fedha
zinamwagika kiasi hiki?
Ningekuwa mimi Mkurugenzi REA, kama fedha kumbe za
kuchezea zipo, ningenunua transfoma moja kwa ajili ya kijiji kimoja.
Kama lengo ni kuweka kumbukumbu sawa, ningeitisha
mkutano na waandishi wa habari na kuwapa sera na mkakati wa kusambaza umeme
vijijini hata kama nisipotaja jina la mwandishi wa makala hayo na gazeti lake.
Hatuwezi
kuchezea fedha kijinga namna hii. Wadau hii kweli Haki? Usikose kusoma makala zangu katika Gazeti lako la Mtanzania kila siku. Hasa kwa makala ya Mgodi Unaotembea kila Jumatano na Jumapili.
No comments:
Post a Comment