Mussa Kitale kulia akiwa na swahiba wake, marehemu Sharomillionea
Na Kambi
Mbwana, Dar es Salaam
MSANII
wa vichekesho na swahiba wa marehemu Hussein Mkiety, maarufu kama
'Sharomillionea', Mussa Kitale, ameendelea kumlilia nyota huyo kwa kusema haamini
kama ni kweli siku zimekwisha na sasa
wanasubiria kumfanyia dua arobaini kipenzi chao, kama anavyofanya kumuombea dua kila mara.
Huu ni Mussa Kitale, Rais wa Mateja
Sharomillionea
alibambwa maeneo ya jiji la Dar es Salaam, akizungumza na wenzake juu ya
kukaribia kwa arobaini ya Sharomillionea inayotarajiwa kusomwa kijijini kwao
Lusanga, Januari nne mwaka huu.
"Kweli
siku zinakimbia jamani, yani tayari tunakwenda kuhitimisha kabisa maisha ya
duniani ya mwenzetu Sharomillionea? Hii ni hatari na hakika Mungu amlaze mahali
pema peponi mpiganaji wetu Mkiety.
"Arobaini
yake itafanyika kijijini kwao Lusanga ikionyesha kuwa katika kipindi hiki
tulikuwa wapweke kwa kukosa uwepo wa Sharomillionea,” alisema Kitale ambaye pia
ni mwimbaji wa Bongo Fleva, akitamba na wimbo wa ‘Hili dude Noma’.
Sharomillionea
alikuwa na ukaribu wa kupitiliza na Kitale, kwani inadaiwa hata siku aliyopata
ajali Tanga, alikuwa aking’ang’ania kusafiri na Kitale aliyekuwa njiani kutoka
Iringa kwenye shoo na marehemu alikuwa akielekea Tanga.
Mbali na
hilo, pia wasanii
hao wamekuwa pamoja kila wakati na kufanya kazi pamoja, hasa baadhi ya nyimbo
walizochanganya sauti au video zao, bila kusahau filamu za vichekesho
walizokuwa pamoja, ikiwamo Mtoto wa Mama, Vituko Show zote, Jini Mahaba, Porojo
na nyinginezo.
No comments:
Post a Comment