Mwanadada Lina Sanga, aakionyesha pozi alipokuwa nchini Marekani kwenyee shughuli zake za muziki.
Na Kambi
Mbwana, Dar es Salaam
MWIMBAJI
wa muziki wa kizazi kipya maarufu kama Bongo Fleva, Linah Sanga, amesema shule
ni jambo jema hivyo kuna haja ya wasanii kujikita zaidi humo.
Kauli ya
Linah inakuja wakati wasanii wengi kuona hakuna haja ya kuendelea na masomo
zaidi ya kujikita zaidi katika sanaa kwa kuangalia mafanikio yao.
Akizungumza
na Handeni Kwetu mwishoni mwa wiki iliyopita, Linah alisema uzuri wa shule ni
pale muziki utakapotupa mkono, hivyo kuweza kuajiriwa popote.
Alisema
kinyume cha hapo, mtu ambaye aliwekeza zaidi kwenye muziki, endapo sanaa
itamtupa mkono, maisha yake yanaweza kuwa magumu zaidi na kuchanganyikiwa.
“Shule ni
nzuri zaidi, natamani hata leo kuendelea kusoma huku nafanya sanaa yangu nikiwa
na malengo ya leo na kesho, hasa muziki utakapokuwa tofauti.
“Hivyo
wasanii twendeni shule na sio kuangalia zaidi muziki, hasa wale vijana
wanaoangalia mafanikio ya watu waliotangulia na kukimbia shule,” alisema Linah.
Linah ni
miongoni mwa wasanii wa kike wenye mafanikio makubwa katika tasnia hiyo huku,
huku nyimbo zilizomuweka juu zikiwa ni Atatamani, Lonely na nyinginezo, wakati
huo yupo chini ya taasisi ya kulea na kukuza vipaji ya Tanzania House of
Talents (THT).
No comments:
Post a Comment