Meneja Mazao wa SASAMUA Estate, Josephat Odhiambo
Na Kambi Mbwana, aliyekuwa Handeni
MENEJA Mazao wa shamba la SASAMUA Estate, lililopo Kwamsisi,
wilayani Handeni mkoani Tanga, Josephat Odhiambo, amewataka watu kuchangamkia
fursa ya kilimo ili waweze kuinua uchumi wao na Taifa kwa ujumla.
Katika shamba hilo, mazao
mbalimbali yanalimwa na kuuzwa ndani na nje ya nchi, zikiwamo nyanya, nanasi,
mboga mboga na mengineyo, huku watu zaidi ya 2500 wakifanya kazi kwenye shamba hilo.
Akizungumza na Handeni Kwetu hivi karibuni katika shamba hilo, Odhiambo alisema
kwamba bila kilimo uchumi wao hauwezi kukua zaidi ya kudidimia katika umasikini
wa kujitakia wenyewe.
Alisema kilimo ni biashara nzuri inayoweza kuleta maendeleo
makubwa, hivyo Watanzania na watu wa Handeni wanapaswa kuangalia kwa umakini
ili wafanye kazi hiyo kwa malengo makubwa.
Nimetoka Kenya
kuja kuifanya kazi hii katika shamba hili, nikiwa na imani kuwa tutauza na
kufanya biashara nzuri ya kilimo, ukizingatia kwamba watu zaidi ya 2500
wanapata maisha kwa kufanya kazi hapa.
Naomba Watanzaniaa wafanye kazi ya kilimo kwa bidii kwa
kuchangamkia ardhi ya kutosha na yenye rutuba, kwakuwa bila hivyo maendeleo
kwao hayawezi kuwa mazuri zaidi ya kukaa kwenye ufukara wa kutisha,” alisema.
Hivi karibuni, Mkuu wa wilaya ya Handeni alifanya ziara
katika shamba hilo
akiwa na baadhi ya walimu wa shule za sekondari katika wilaya hiyo, paamoja na
baadhi ya wanafunzi kutoka shule mbalimbali kwa ajili ya kujifunza kilimo.
No comments:
Post a Comment