MAMBO
FULANI MUHIMU
Mapenzi yenye raha kwa wawili hawa
Na
Kambi Mbwana, Dar es Salaam
WAHENGA
hawakukosea waliposema ‘kikulacho kinguoni mwako’. Msemo huu muhimu kabisa ni
kati ya ile inayotumiwa kwa nyakati tofauti.
Wazee
wetu walifahamu hilo, kitu kilichowafanya
waiweke kinywani mwao wakiwa na lengo la kutoa elimu kwa jamii, baada ya kuona
marafiki wanaojuana hugeuka kama kinyonga na
kufanya wanavyojua wenyewe.
Hii
ni mbaya sana.
Kwa bahati mbaya aina hii ya maisha inatumiwa na watu wengi, jambo linalowafanya
washindwe kuaminika mbele ya hadhira.
Msemo
huo naweza kuutumia hata katika mambo ya kimapenzi. Baadhi ya watu wasiokuwa na
akili timamu, hujikuta wakiwabadilikia marafiki zao na kuwatamani wapenzi au
wake zao.
Wale
wanaoaminiwa sana
na jamaa zao, hutumia muda huo kujiwekea mazingira ya kuwasaliti marafiki zao
hao, baada ya kufanikiwa kuwarubuni wenzao.
Huo
ndio ukweli. Wapo ambao hadi leo wanatumia nafasi hiyo kwa kujiingiza kwenye
uhusiano wa kimapenzi na wake au wapenzi wa marafiki zao.
Ni
wengi mno. Wanatumia muda huo kujichanganya kimwili kwa watu hao, tena katika
nyumba au vitanda vya hao maswahiba zao.
Hao
ndio watu bwana. Maana watu ni wengi ila binadamu ni wachache. Hao kufanya
uchafu wa kimapenzi na wapenzi wa wenzao ni rahisi kwao.
Hawaoni
uchungu ama kinyaa huku wakijifanya wajuzi wa mapenzi kwa kutoa mitindo ambayo
wanajua fika waume hao hawajawahi kuipata kwa wake watu wao.
Huwateka
kabisa kiakili na kifikra. Hubarikiwa utundu wa kujihusisha na mapenzi na
wasichana hao ambao, anajua kuwa ni mali za watu.
Sio
wanaume tu. Hata wanawake mandumilakuwili ni wengi mtaani kwetu. Yule msanii wa
Bongo Fleva, Samu wa Ukweli alisema hata kwetu wapo.
Tena
wanawake ndio kabisa. Baadhi yao
huomba ruhusa kabisa kwa marafiki zao wakitaka kutoka ‘out’ na mashemeji zao.
Wakifika
huko huwafanyia vituko kwa kujishaua kwa mengi, ikiwamo kurembua macho ama
mitego mingine ambayo ni wanaume wachache humudu kuiugundua na kuvaa ujasiri wa
aina yake.
Wengi
wao huingia mtegoni na kushindwa kuvumilia, hivyo kujikuta hisia zao zikitamani
kulala nao kitanda kimoja kwa ajili ya kuvunja amri ya sita.
Ndio
hapo unapotakiwa kusoma alama za nyakati. Hutakiwi kumuamini rafiki yako hata
kidogo. Mambo ya mume au mpenzi wako lazima ufanye wewe mwenyewe maana siku
hizi waaminifu ni wachache.
Lazima
ujuwe kwamba ukimpa nafasi rafiki yako kwa mambo ya mapenzi, huenda
ukapinduliwa na nyumba yako akaenda kuishi yeye.
Wapo
wengi mtaani kwetu na huko kwenu pia. Baadaye hulia na kusaga meno. Hudanganya
kwa mengi likiwamo ‘sijamuita mumeo kaja mwenyewe’.
Hapo
jua huna chako muungwana. Hivyo lazima ujuwe mtu wako wa karibu ana uwezo wa
kuwa mbaya yako, endapo umemuachia nafasi kubwa kwa mtu wako, hadi kumuingiza
mtegoni.
Jua
kabisa mtu wako ana uwezo wa kunyakuliwa kulingana na mwenekano wake. Iwe ni
uvaaji, usomi wake, ama uwezo wake wa kifedha.
Haya
na mengineyo yanaweza kuifanya ndoa ama uhusiano wako ushindwe kuendelea
kutokana na wachokonozi hao kuingia kwenye malavidavi yako.
Hakuna
njia ya mkato zaidi ya kuhakikisha kwamba rafiki yako, haingii zaidi kwenye
ukaribu na mume au mke wako, pamoja na wale wapenzi.
Kuwa
mkali, maana siku zote kunguru muoga hukwepesha ubawa wake.
Ingawa baadhi yao huwaachia waume zao
ama wake zao nafasi ya kujenga mazoea ya ajabu kwa wenzao, ila hulia kilio cha mbwa.
Ni
pale wanapong’amua kwamba mtu wake ameanzisha uhusiano wa kimapenzi na rafiki
yake na kuufanya uhusiano wao uyumbe kama sio
kuvunjika.
Akija
ndani asubiri sebuleni ila sio kuingia hadi chumbani, huku akijua wewe upo
mbali. Ikiwezekana asikae ndani kwa madai anakusubiri wewe.
Ndio
ukweli huo. Bila kuwa makini utaibiwa na hao hao marafiki zako, maana uadilifu,
uaminifu kwenye uhusiano umekuwa adimu kuliko fedha.
kambimbwana@yahoo.com
0712
053949
0753
806087
No comments:
Post a Comment