Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
Kocha mpya
wa Simba, Mfaransa, Patrick Liewing pichani, aliyeshika nguo nyekundu mkononi, amewasili leo saa saba za mchana kwa ajili ya
kuinoa timu ya Simba. Uongozi wa Simba, kwa kupitia Katibu Mkuu wao, Evodius
Mutawala, alikuwa miongoni mwa wadau wa michezo waliompokea Liewing katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere.
Kocha
huyo anawasili huku akiikuta timu ya Simba ikiwa chini ya Jamhuri Kihwelo
Julio, kocha ambaye amekuwa na mapenzi makubwa na klabu hiyo kila wakati kwa
kitendo chake cha kukubali kuinoa timu hiyo.
Mengi juu
ya ujio wa kocha huyo raia wa Ufaransa, yatasikika baada ya kufanya mazungumzo
ya mwisho na kuingia makubaliano rasmi ya kuinoa Simba, yenye kipindi kikubwa
cha kurudisha imani kwa wapenzi na wanachama wao.
Simba
ilimaliza mzunguuko wa kwanza wa ligi ya Tanzania kwa kushika nafasi ya
tatu, nyuma ya timu ya Yanga na Azam FC.
No comments:
Post a Comment