https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543


Recent Post

Tuesday, December 18, 2012

Uhondo wa Skylight Thai Village Masaki

Muziki  mtamu jamani. Hawa ni baadhi ya mashabiki wa bendi ya Skylight wakifanya vitu vyao jana Masaki, jijini Dar es Salaam. Unaambiwa kujuana mahome bwana. Club tumekuja kustarehe. Huyu dada wa nyuma mstari wa mbele anacheza ngoma gani? Picha hii nimeipenda sana na ndio maana kamera ya Handeni Kwetu haifanya makosa kuifotoaaa..

Hapa hakuna kuangaliana usoni. Jamaa huyu akishindwa kujizuia na kuanza kukata mauno katika onyesho la bendi ya Skylight jana usiku.
Mwimbaji wa bendi ya Skylight akifanya vitu vyake. Nikueleze kitu. Huyu jamaa anayecheza kushoto kwa Mary Lucas, mfuko wake wa nyuma una nini? Ninyamaze mieeeeee.
Wazimu wangu ukinipanda hata moto siangalii. Hapa watu wakifanya vitu vyao. Muziki mtamu jamani. Duh? Huyu dada na kaka walivyoshikana sasa. Kule wengine wanapinda mugongo.
Wanamuziki wa bendi ya Skylight wakifanya vitu vyao jukwaani.


No comments:

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...