Mwenyekiti wa CCM, Jakaya Mrisho Kikwete, akipeana mikono na watoto, katika moja ya shughuli za kichama.
Na Rahimu Kamb, Handeni
MWENYKITI wa Chama Cha Mapinduzi CCM wilayani Handeni mkoani
Tanga, Athumani Malunda, amejigamba kuwa wilaya yao itaendelea kuwa ngome imara ya chama chao
kutokana na wananchi wao kuwaheshimu na kukithamini na kukiweka madarakani.
Malunda aliyasema hayo mwishoni mwa wiki mjini hapa,
akizungumzia pia mikakati ya chama katika kusimamia watendaji wao kwa ajili ya
kuleta maendeleo kwa Handeni na Tanzania
kwa ujumla.
Akizungumza na Handeni Kwetu, Malunda alisema kwamba
historia inaonyesha kuwa wilaya yao
ni ngome imara ya CCM, hivyo uongozi hauwezi kukubali kuiondosha sifa hiyo
muhimu kwa Taifa lao.
Alisema CCM Handeni na Taifa kwa ujumla watashiriki kwa
karibu kuwakumbusha viongozi wao kwa ajili ya kuhakikisha kuwa wananchi wao wanapata
maisha bora jambo litakalowapa imani zaidi.
“Tanzania
imekuwa ikikabiriwa na siasa za vyama vingi lakini kwetu tunashukuru kuwa
wananchi wetu ni waelewa zaidi na wanakipenda chama chao, ndio maana hivyo
vyama vya upinzani havina nguvu hapa kwetu.
“CCM imekuwa ikiongoza kwa mafanikio makubwa pamoja na
kutatua kero za wananchi wao siku hadi siku, hivyo sioni sababu ya Handeni
kuondoka kwenye utawala wa CCM na kuwaachia wapinzani, wasiojitambua na
wasiokuwa na sifa ya kuwaongoza Watanzania, tukiwapo sisi Handeni,” alisema
Malunda.
Maneno ya Malunda yamekuja katika kipindi ambacho baadhi ya
Watanzania wamekuwa kwenye nafasi ngumu hasa kwa kuaminishwa kuwa CCM
imeshindwa kutatua kero zao, hivyo wanastahili kuongozwa na wapinzani.
No comments:
Post a Comment