Steve Nyerere kulia akiwa na Wema Sepetu
Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
MKALI wa filamu hapa nchini,
Steve Nyerere amedaiwa kushika nafasi ya kwanza kwa wasanii wanaowaunganisha na
mapedeshee warembo wanaofanikiwa katika game la filamu Bongo.
Kutajwa huko kumekuja wakati
ambapo kashfa hiyo imezidi kushika nafasi katika sanaa, huku wadau wakisema
Steve Nyerere ni kiboko kwa kuwaunganisha na watu wasanii wa kike.
Habari kutoka kwa mtu wa
karibu na msanii zinasema kwamba mkali huyo mwenye manjonjo mengi, alisema watu
hao wamekuwa wakipitia zaidi kwa jamaa huyo ili wawanase warembo.
Alisema jambo hilo linamuweka katika
mazingira magumu msanii huyo, ambaye anajulikana pia kwa uwezo wake kuigiza
sauti za watu maarufu, akiwamo Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere.
"Yule jamaa anajulikana kwa
kazi hiyo, lakini sidhani kama ina ukweli hasa ukizingatia kwamba baadhi yao wanasema hivyo
wakiangalia ukaribu wa msanii huyo na wasanii wa kike.
"Kwa mfano watu kutoka mikoani
wenye uwezo mkubwa kifedha, wanadaiwa kuwa wakitaka ukaribu wa aina yoyote na
wasanii wa kike wa Tanzania
wenye majina hupitia kwake,” alisema mpashaji huyo ambaye naye alitembelea
katika mikoa mbalimbali ya Tanzania,
wasanii hao wa Bongo Movie walipofanya ziara.
Kule mikoani, Steve Nyerere
ndio alikuwa kinara wa kushika kipaza sauti na kuwaita wasanii waliokuwapo
kwenye msafara huo wa Fiesta 2012, akiwawataka pia wacheze jukwaani.
No comments:
Post a Comment