CCM
Handeni isicheze na fikra za walalahoi
Mkuu wa Mkoa Tanga, Chiku Galawa
Na Kambi
Mbwana, Dar es Salaam
NI
kawaida yangu sasa kila ninaposafiri kwenda mahali popote, ninaporejea huchukua
walau muda mdogo kuandika changamoto zinazowasumbua Watanzania.
Katika
kuandika kwangu, huwa pia siangalii chama wala taasisi yenye kushindwa
kuwasimamia kikweli Watanzania, nikiamini dosari hizo zitaongeza umasikini wa
raia wake.
Mkuu wa Wilaya Handeni, Muhingo Rweyemamu
Ni kweli.
Na katika hilo,
baadhi ya wadau wameshindwa kunielewa mtazamo wangu mara moja, huku wakishindwa
kuniweka katika kundi la chama Fulani.
Mwenyekiti wa CCM Handeni, Athumani Malunda
Kwa
mfano, wapo wanaonisema wakidhani mimi ni shabiki wa chama Fulani, iwe Chama
Cha Mapinduzi (CCM), Chama Cha Wananchi CUF, Chama Cha Demokrasia na Maendeleo
chadema na vinginevyo vinavyosajiliwa kila uchao.
Meseji
zinazokosoa au kusifia nazipata kwa wingi, huku baadhi yao nikiwajibu kuwa, sioni sababu za kuweka
chama changu mbele, hasa ninapojadili maslahi ya Watanzania.
Inaweza
kuwa ni kweli mimi ni mfurukutwa kama wanavyosema baadhi yao,
lakini sio tiketi ya kukiacha chama hicho kiende kama
mbuzi waliopotea machungaji kwa kushindwa kuwakosoa viongozi waliokuwa kwenye
uongozi.
Ingawa
nitakuwa mwana CUF, Chadema au TLP. Lakini ninapoona mapungufu, sibaki nyuma
kusema, ndipo hapo watu wanaposhindwa kuelewa nipo mlengo gani?
Sio lengo
langu kuelezea aina ya maisha yangu na changamoto zangu, maana sijaandika
makala haya kwa ajili hiyo.
Lengo
langu ni kuutaka uongozi mzima wa CCM wilayani Handeni, mkoani Tanga na Tanzania kwa
ujumla kuangalia sera na changamoto zinazoweza kuwapatia maisha bora.
Endapo
maisha bora yatapatikana kwa wilaya hiyo, hakika hizi shangwe na majigambo kuwa
CCM itaendelea kutawala milele wilayani humo zitafanikiwa.
Kwanini
nasema hivi? Kwa miaka 51 sasa ya Uhuru Chama Cha Mapinduzi CCM kimekuwa imara
kwa wilaya nzima ya Handeni, hasa kwa wananchi wake kukiweka madarakani.
Lakini,
licha ya wananchi hao kuipa dhamana ya kuongoza katika chaguzi mbalimbali,
lakini kuna njia nyingi zinazowapa ahueni CCM katika jimbo hilo linalotawaliwa na Mbunge wa Handeni,
Abdallah Omari Kigoda.
Kwa
sababu hiyo, nashawishika kusema kuwa bila mipango madhubuti kutoka kwa
viongozi wa wilaya, mkoa na Taifa kwa ujumla, kuna siku CCM Italia kilio cha
mbwa.
Nasema
hivyo kwasababu ni ngumu sana kumlinda mbwa mwenye
njaa. Na hakika hakuna fundi wa aina hiyo. Mbwa mwenye njaa hawezi kutulia
nyumbani kwao.
Ili akae nyumbani, lazima mfugaji amfunge nyororo mara kwa
mara kwa kujua wakati wowote atakimbia. Huu ndio ukweli. Wanachama na
Watanzania wanaoshi Handeni ni sawa na mbwa mwenye njaa.
Kukaa
katika chama hicho miaka nenda rudi ni hadithi. Hatuwezi kuwalinda wananchi
wasikipige chini chama hiki kikongwe kama hakuna juhudi za maisha yao kuwekwa sawa.
Viongozi
wa Chama na serikali kwa pamoja wakae na kusikiliza malalamiko kutoka kwa
wananchi wao. Matatizo ya uvamaizi wa mashamba yao yafanyiwe kazi.
Matatizo
ya maji nayo yasipofanyiwa kazi hakika wananchi lazima waichukie CCM. Nasema
hivyo kwasababu nimekuwa nikitembelea wilayani humo mara kwa mara.
Nashukuru,
katika kutembea kwangu huko, sikuwa na lengo la kuangalia matatizo tu kwa ajili
ya kuyaanisha kwa lengo tofuati kama inavyofikiriwa na baadhi yao.
Kutembea
kwangu huko kuna lengo la kuangalia namna gani wananchi wa Handeni maisha yao yanakuwa mazuri kwa
kupitia uongozi uliopo madarakani.
Nilipokuwa
Handeni niliweza kufanya mazungumzo na baadhi ya viongozi wa chama na serikali.
Nashukuru,
maana nilipewa nafasi ya kusikilizwa namna gani wananchi wanaweza kushirikiana
na viongozi wao kwa ajili ya maendeleo ya Handeni.
Hata
hivyo, mazungumzo hayo yamekuwa yakizungumzwa mara kwa mara, huku baadhi yao zikishindwa kufanyiwa
kazi. Kama hivyo ndivyo, yoyote anayeishi
maisha mazuri na familia yake huku raia wake wakilala njaa huyo anatia shaka.
Wimbo wa
kero ya maji katika wilaya ya Handeni unaweza kuachwa kama
sera na mipango itachukuliwa.
Ndio,
baada ya kuhanagaika sana,
hatimae miezi michache ijayo, wananchi wataweza kuzunguukwa na barabara ya
lami.
Hadi
sasa, ukitoka Dar es Salaam
kwenda Handeni kwa kuingilia Mkata ni lami kwa lami.
Lakini
pamoja na hayo, ile nyingine ya kotoka Korogwe kwenda Handeni nayo inaendelea
kujengwa, jambo litakalokuwa na faida kubwa.
Tusiishie
hapo. Tupige hatua ya mbele zaidi. Lazima tujuwe kuwa barabara hizo zinatumiwa
kimaendeleo. Watu wa Handeni waishi kwa kufanya kazi ipasavyo ikiwamo wale
wajasiriamali wanaoishi ndani na nje ya Handeni.
Serikali
ya CCM ilijuwe hilo,
maana mambo yasipoangaliwa kwa kina, watu kutoka nje wanaweza kunufaika na
barabara hizo, huku wenyewe wakidoa macho.
Utashangaa
kwanini nasema serikali. Hii ndio kila kitu. Hata kwa kupitia mfuko wa Jimbo,
sehemu ya mfuko huo inaweza kutumika kuendeleza wakulima au wajasiriamali.
Kama hivyo sivyo, basi pia kuwe na mipango ya kuwasimamia watu
na kuwaendeleza katika kilimo maana ndio uti wa mgongo. CCM isibaki kusema tu
chama kitatawala milele kama alivyosema
mwenyekiti wake wa wilaya, Athumani Malunda, alipozungumza na Mtanzania
wilayani humo.
Kila
mwana Handeni wakiwamo viongozi na wananchi wao wafanye kazi kwa ushirikiano
kwa ajili ya watu wote.
Mwenyekiti
wa wilaya na Katibu wake wawe wakali zaidi kusimamia watendaji, wakimpa
ushirikiano Mkuu wao wa Wilaya, Muhingo Rweyemamu, aliyeingia Handeni kwa miguu
yote.
Tusiwe
watu wa kutangaza miradi ya maendeleo na kushindwa kuiendeleza. Wakati mwingine
huwa nasema, sera za kwenye makaratasi ni tatizo kubwa.
Wengineo
wamekuwa wakiumizwa sana
na maneno yangu, lakini huo ndio ukweli wa mambo. Nausema kwakuwa tunafanya
yale ya kuiendeleza nchi yetu.
Kama hatutaelezana ukweli, ina maana kupiga hatua ya mbele
zaidi ni kujidanganya tu. Tufanye siasa lakini pia wakati mwingine tuwe na sera
zinazotekelezeka.
Sio
Handeni tu, bali pia wilaya zote zilizopata viongozi wao wa CCM wafanye kazi
imara ya kuendeleza maendeleo yao.
Huo ndio
ukweli. Lakini tusipofanya hivyo, kuwang’ang’ania wananchi waendelee
kukiheshimu chama chao ni kumpigia mbuzi gitaa wakati tunajua hawezi kucheza.
Kwa
Tanzania ya leo inayokua kidemokrasia na kukua kwa vyama vya siasa vya
upinzani, kuna siku wananchi wake watajuwa kwanini chama tawala kinastahili
kukaa pembeni.
Watafanya
hivyo kwasababu tangu walipozaliwa, wameikuta CCM katika maeneeo yao, huku wakiendelea kubaki kama
walivyo, wakati wenzao wanapiga hatua.
Wilaya
hii ya Handeni kutokuwa na nguvu ya vyama vya upinzani sio matokeo mazuri kwao,
maana wakishaelewa kuwapata ni kazi ngumu mno, hivyo CCM iliangalie hilo.
Nalisema
hili kwasababu ndio maisha yangu ya kawaida kuhubiri ukweli, huku nikijweka
kando na fitina kwa kusifia kila linalofanywa hata kama
najua ni baya.
Na
ikitokea wapinzani wanakuwa na sauti Handeni kama
ilivyokuwa katika baadhi ya maeneo, viongozi waliopo wataonyesha udhaifu wao
kwa kushindwa kuelewa kuwa siku zote mipango ya kushinda vita yoyote ni
kumfuata adui mbele na sio kusubiri aje kukuvamia, maana atatuamia silaha zako
mwenyewe kukumaliza.
0712
053949
0753
806087
No comments:
Post a Comment