Zena Chande mwandishi wa
Gazeti la Habari Leo, ni mgombea
Na Kambi Mbwana, Dar es
Salaam
UCHAGUZI wa viongozi
wapya wa Chama cha Mpira wa Miguu wa Wanawake Tanzania (TWFA) unafanyika kesho
(Desemba 19 mwaka huu) kwenye hoteli ya Midlands mjini Morogoro.
Msemaji wa Shirikisho la
Mpira wa Miguu nchini (TFF), Boniface Wambura, alisema Kamati ya Uchaguzi ya
TWFA ikiongozwa na Mama Ombeni Zavala ndiyo itakayoendesha uchaguzi huo chini
ya usimamizi wa Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania
(TFF).
Wagombea katika uchaguzi
huo ni Isabela Kapera, Joan Minja na Lina Kessy wanaowania uenyekiti, Rose
Kissiwa (mgombea pekee wa nafasi ya Makamu Mwenyekiti), Amina Karuma na Cecilia
Mkafum (wanawania ukatibu mkuu).
Wengine ni Zena Chande
(mgombea pekee wa nafasi ya Mjumbe Mkutano Mkuu wa TFF) na Sophia Charles na
Triphonia Temba wanaowania ujumbe wa Kamati ya Utendaji ya TWFA.
No comments:
Post a Comment