Mwenyekiti wa Yanga, Yusuph Manji
Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
SHIRIKISHO la Soka nchini (TFF),
limesema kuwa klabu 14 zinazoshiriki Ligi Kuu ya Vodacom zimesusia kucheza hatua
ya pili ya Ligi hiyo itakayoanza Januari 26 mwakani hadi zitakaporejeshewa
fedha zao zilizochukuliwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kutoka kwenye
moja ya akaunti za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).
Mwenyekiti wa Simba, Ismail Aden Rage
Novemba 23 mwaka huu, TRA kwa
uwezo ilionao kisheria iliielekeza benki ya NMB kuilipa fedha hizo (sh.
157,407,968) kutoka kwenye moja ya akaunti za TFF ikiwa ni Kodi ya Lipa Kama
Unavyopata (PAYE) kutoka kwenye mishahara ya waliokuwa makocha wa timu za Taifa.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotuma
kwenye vyombo vya habari na Ofisa Habari wa TFF, Boniface Wamburaa, ilisema
kuwa uamuzi wao huo unatokana na kujua kuwa Serikali ndiyo inayolipa mishahara
ya makocha wa nje moja kwa moja kwenye akaunti zao, huku ikiacha kukata PAYE kwa
mishahara hiyo na kufikia kufikia malimbikizo ya sh. 157,407,968.
TFF bado inaendelea na mazungumzo
na pande husika (Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kwa upande
mmoja na TRA kwa upande mwingine) ili fedha hizo zirejeshwe kwani zilitolewa na
mdhamini wa Ligi Kuu (kampuni ya Vodacom) kwa ajili ya maandalizi ya timu hizo
tayari kwa mzunguko wa pili wa Ligi hiyo.
Katika hatua nyingine, TFF
imesema kuwa Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) litamtuma nchini ofisa
wake Abbas Sendyowa kukagua viwanja na hoteli ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa
utaratibu wa klabu kupata leseni zitakazoziwezesha kushiriki michuano
inayoandaliwa na CAF katika ukanda wao.
Ofisa huyo kutoka Uganda atawasili
nchini Januari 7 mwakani ambapo anatarajiwa kukamilisha kazi hiyo Januari 14
mwakani na baadaye kupeleka ripoti yake CAF.
Aidha, Kamati ya Uchaguzi ya
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imekubaliana na uamuzi wa Kamati ya
Uchaguzi ya Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Rukwa (RUREFA) kumuondoa Nazarius
Kilungeja kugombea uenyekiti katika uchaguzi wa chama hicho.
Kutokana na uamuzi huo, Kamati ya
Uchaguzi ya TFF imeiagiza Kamati ya Uchaguzi ya RUREFA kuendelea na mchakato wa
uchaguzi huo kama ilivyopangwa awali.
No comments:
Post a Comment