Mbwana Samatta, akiwa kwenye usafiri anaotumia nchini Kongo. Picha kwa hisani ya mitandao.
SIWEZI KUVUMILIA
Na Kambi Mbwana, Dar
es Salaam
MBWANA Samatta na mwenzake Thomas Ulimwengu hawana sababu
za kuidharaau timu ya Taifa, Taifa Stars, hata kama
wamechoka au wanamatatizo ya kiafya.
Sina lengo la kusema kwamba wachezaji hao wanaokipiga
katika klabu ya TP Mazembe ya nchini Kongo wacheze tu hata kama ni wagonjwa,
bali matatizo yao
hayo yasemwe na wataalamu wa tiba wa Stars na kocha wao.
Kwa miezi kadhaa sasa wachezaji hao, hasa Samatta amekuwa
kwenye kashfa ya kuidharau timu yake bila sababu za Msingi na kuanza kuleta
wasiwasi kwa maendeleo yake.
Kwanini nasema hivyo. Timu ya Taifa ndio jicho la kuonwa
wachezaji wengi wa ligi wa ndani na wale waliokuwa nje ya nchi.
Wadau wa soka wanaweza kuangalia zaidi wachezaji wa timu
ya Taifa, kuliko wale wanaocheza kwenye vilabu. Huu ndio ukweli. Hata Samatta
mwenyewe anajua kuwa mafanikio yake aliyokuwa nayo sasa yamechangiwan kwa kina
na Stars.
Ikiwa chini ya Marcio Maximo kabla ya kumaliza mkataba
wake na kurudi kwao Brazil,
Samatta aliweza kutumika kwenye Stars hiyo na kutangazwa sana.
Kama hivyo ndiyyo, leo hii Samatta anapata wapi jeuri ya
kuidharau Stars hata kama iwe haina tija
kwake? Stars ni timu ya Watanzania wote, wakiwamo wale wa Simba na Yanga.
Mchezaji anayeweza kuidharau timu ya Taifa, ina maana huyo
analidharau Taifa lake
lote. Wachezaji wengi wa
nje wakiwamo walioendelea wanazithamini timu zao.
Mchezaji asipoitwa kwenye timu yake ya Taifa analia. Hana
furaha zaidi ya kuumizwa na matokeo hayo. Tunashuhudia mafanikio yao yanavyochangia kuleta
tija kwa soka lao.
Hivi karibuni niliwahi kukutana na mlango wa Stars, Juma
Kaseja katika matukio ya Kitaifa. Kaseja alinikimbilia nikiwa na wadau wengine
wa soka, akisema kuwa hadi leo ana gazeti la Mtanzania, ikiwa na ukurasa huu wa
Siwezi Kuvumilia akisema ulimuandika vibaya kuwa hana mapenzi na Stars.
Kaseja alisema sio kweli bali wakati naandika makala yale,
alikuwa ameumia taya. Namimi bila kuleta kelele, nilimwambia kwakuwa upo kwenye
shughuli za Taifa, ukirudi tuonane tulijadili hilo.
Nilifanya hivyo kwa kulinda heshima yake. Ningeweza
kumwambia pale kuwa, kama uliumia taya saa
chache ulipoitwa na Stars, ilikuwaje saa kumi jioni ufanye mazoezi na timu yako
ya Simba jijini Tanga?
Ningemuuliza tena, kwanini uliwahi kutupwa nje ya Stars
kwakuwa ulionekana ukishangilia baada ya Stars kubugizwa mabao 4-0 kutoka
katika moja ya timu za Afrika, huku golini akiwa ni Ivo Mapunda?
Hakika siwezi kuvumilia. Lakini kwake nilijizuia kwakuwa
maswali hayaa ningemuuliza Kaseja huenda ningemuumiza zaidi, ukizingatia kwamba
ndio ameanza tena kurudi kwenye kiwango cha kuitumikia Stars, ikiwa na Kim
Poulsen.
Nilichoshukuru, Kaseja ni miongoni mwa wasomaji wa safu
hii ya siwezi kuvumilia kama walivyokuwa
Watanzania wengine, nikiamini siandiki bila kufanya uchunguzi.
Kama hivyo ndivyo, Samatta na Ulimengu hawana uwezo wa
kuikataa timu yao
ya Taifa. Katika mchezo wa juzi dhidi ya Zambia
yenye vichwa kama vole Christopher Katongo,
Stars iliweza kuibuka na ushindi wa bao 1-0.
Bao hilo
lilifungwa na winga machachari, Mrisho Ngassa. Kama
vijana hao wangekuwa muhimu zaidi, Stars ingefungwa na wanapokuwa wao ishinde.
Katika mchezo huo wa juzi Jumamosi, kuna mashabiki
walikuwa na mabango yanayosema Who’s Samatta. We have Ngassa. Kwa tafsili
isiyokuwa rasmi, mdau huyo anauliza.
Samatta ni nani? Tunaye Ngassa na kweli umuhimu wake
unaonekana uwanjani kwa kuipachikia bao pekee na la ushindi timu yake ya Taifa,
Taifa Stars.
Huu ndio ukweli. Mchezaji yoyote anayeweza kuikataa timu ya
Taifa, huyo anashangaza sana.
Wakala yoyote hawezi kusajili mtu bila kuangalia mafanikio yake uwanjani na
kwenye timu ya Taifa.
Sasa kama hivyo ndivyo, kuna kila sababu ya wachezaji wetu
wa Tanzania
kuwa na akili timamu katika utendaji wa kazi uwanjani kwa kuangalia harakati
zao kimaendeleo.
Vinginevyo, wachezaji wa aina hiyo watakuwa kwenye wakati
mgumu, maana mafanikio yao
zaidi huenda yakapatikana kwenye timu za Tanzania.
Makala ya Siwezi Kuvumilia hutoka kila Jumatatu katika Gazeti la Mtanzania...
Makala ya Siwezi Kuvumilia hutoka kila Jumatatu katika Gazeti la Mtanzania...
0712 053949
0753 806087
No comments:
Post a Comment