Ray C ni mmoja wa waathirika wa dawa za kulevya
Na Kambi
Mbwana, Dar es Salaam
HARAKATI
za kupambana na utumiaji wa dawa za kulevya ni ngumu sana katika vizazi vyetu vya leo,
vinavyojumuisha pia wasanii nchini. Hawa ni watu makini, ila wameingia kwa kasi
mno katika utumiaji wa dawa za kulevya.
Ramadhani Masanja (Banza Stone mwimbaji wa muziki wa dansi.
Nakumbuka
miaka minne iliyopita, msanii ambaye pia ni mwanasiasa kutoka Chama Cha
Wananchi (CUF), Kalapina, alitunga wimbo uliokwenda kwa jina la ‘Hip Hop bila
Madawa’.
Wimbo huu
ulifanya vizuri, maana ulijaribu kuelezea matatizo na wasanii wale
waliojihusisha na utumiaji wa dawa za kulevya.
Sina
uhakika kuwa kati ya wale waliotajwa kwenye wimbo huo ni kweli wanatumia dawa
za kulevya ama walitajwa kama wawakilishi tu
wa wasanii.
Sitaki
kuwataja tena katika makala haya, maana kwa wasanii na wanaofuatilia kwa karibu
sanaa, wimbo huo na watajwa wanawajua.
Hii ndio
hoja yangu. Hoja ambayo inaelezea kwa kirefu kadhia ya wasanii wa Tanzania
kujiingiza kwa kasi katika utumiaji wa dawa za kulevya.
Katika
kuliangalia suala hilo, kama
ilivyokuwa kwa sanaa hii mara nyingi kuigwa kutoka nje, wasanii wanaona kuna
umuhimu wa kuiga kila kitu, ikiwamo utumiaji wa dawa za kulevya.
Haya ni
matatizo makubwa. Kama wasanii wetu wanaotegemewa kuelimisha jamii nao wanakuwa
waathirika wakubwa, Tanzania
inaelekea wapi.
Mimi ni
miongoni mwa Watanzania walioshtushwa na habari za msanii wa kike nchini,
Rehema Chalamila, maarufu kama Ray C.
Nilishtushwa
ndio, maana habari za yeye kutumia dawa za kulevya zilianza kuvuma zamani, hadi
kusaidiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete.
Pamoja na
hayo, Ray C ni mmoja kati ya Watanzania wengi wanaoingia kwenye utumiaji wa
dawa hizo. Wapo wengi wanaoingia kwenye matumizi hayo yasiyokuwa na faida
yoyote ile.
Hii ni
aibu kubwa. Hatuwezi kuvuna chochote kama
wasanii pamoja na jamii yapo wataona starehe nzuri ni dawa za kulevya.
Nikiambiwa
nielezee athari za dawa za kulevya, kwa msanii kama
Ray C, naweza kusema kuwa matumizi hayo yamesababisha pia kutaifisha kipaji
chake.
Ray C
yule aliyekuwa anajituma jukwaani pamoja na kuachia nyimbo nzuri zilizotikisa
katika vituo vya redio, si huyu wa leo anayeisubiri hisani ya raisi.
Haya ni
matatizo makubwa. Nadhani kwa kulijua hilo,
wasanii pamoja na jamii yao
kwa ujumla wanatakiwa jiangalie mara mbili. Dawa za kulevya hazina faida zaidi
ya kuwapa athari kimaisha.
Dawa za
kulevya si tu ni hatari kwa afya za watumiaji, bali pia zinauzwa kwa bei ghari
kupita kiasi. Mtumiaji kwa siku anatakiwa asiwe na kiasi kisichopungua 20,000
kwa watu wenye kipato cha chini.
Mbaya
zaidi, kadri mtu anavyozea dawa hizo, gharama yake inazidi kupanda mara dufu,
hivyo fedha zake nyingi kuingia katika starehe hizo zisizokuwa na mpango wowote
kwa jamii yetu.
Ukiangalia
kwa haraka, utagundua wasanii wengi wanaishiwa nguvu kwasababu ya janga hilo. Muda wao mwingi
wanaitumia katika sterehe na kupoteza pia gharama zao.
Wengine
sauti zao zinatoweka baada ya kujiingiza katika utumiaji huo wa dawa za
kulevya. Ni hatari tupu. Nadhani wasanii wenyewe wanatakiwa wajiangalie kwa
ajili ya kuboresha maisha yao.
Kila
msanii lazima ajuwe kuwa utumiaji wa dawa za kulevya si ujanja bali ni ujinga
na hasara kwa maisha yake ya sanaa. Hakuna cha maana anachoweza kukipata katika
kuingia kwenye anasa hizo.
Kinyume
cha hapo atapata hasara kubwa kifedha pamoja na kukosa mbinu za kujiendeleza
kisanaa. Huo ndio ukweli.
Harakati
za kupambana na dawa za kulevya ziendelezwe kwa kuwaelimisha jamii kwa kupitia
wasanii wetu na sio kuanzia kwa waelimishaji wetu.
Sanaa ni
kioo cha jamii. Lakini kwa bahati mbaya baadhi ya wasanii wamekuwa
wakisumbuliwa na ujinga wa kuiga hata kula kinyesi. Huu ni ujinga wa karne.
Wasanii wetu wajiepushe na matumizi haya mabaya na yanayoharibu vipaji vyao kwa
namna moja ama nyingine.
Huu ndio
ukweli. Tuukubali kwa ajili ya kuwa na kizazi chenye kujitegemea na mafanikio
makubwa kutokana na kazi zao na sio kupoteza muda wao kutumia dawa za kulevya
zinazonunuliwa kwa gharama kubwa mno.
0712
053949
0753
806087
No comments:
Post a Comment