Nchini Tanzania kuna fursa nyingi sana za uwekezaji katika sekta ya ufugaji
nyuki hasa katika nyanja zifuatazo ambazo ni viwanda vya kutengeneza vifaa vya
ufugaji wa nyuki, ambavyo ni mizinga ya nyuki, mavazi ya kinga, mashine ya
kukandamiza na ya kukamulia asali, vifaa vya kuhifadhia asali na vifaa vya
kuchujia nta.
Pia alivitaja viwanda
bidhaa zitokanazo n anta ambavyo vinajumuisha shughuli za biashara kama vile,
utengezaji wa mishumaa, matumizi ya nta kama
kiambato muhimu katika dawa, vipodozi, mafuta ya kulainishia mitambo, polishi na
mengineyo.
“Pia viwanda vya bidhaa zitokanazo na asali kwa kutengeneza pombe,
mvinyo, kiambato muhimu katika dawa, kikolezo kitamu katika maji matatu ya
matunda/juisi, mikate, biskuti, na uhifadhi wa chakula.
“Aidha kuna uchavushwaji unaofanywa na nyuki na kuboresha
mazao yatokanayo na mimea ya kupanda mashambani na mimea ya asili, ukizingatia
kwamba nyuki ni wazuri katika uboreshaji wa wingi na ubora wa matunda na
mbegu,” alisema Gladness.
Mkurugenzi huyo msaidizi wa nyuki anasema kwamba bidhaa hiyo pia
hutumika kama pembejeo katika mashamba kwa
kuongeza uchavushaji wa mimea ya asili na ya kupandwa mashambani.
Anatolea mfano jinsi
makundi ya nyuki yanavyoweza kukodishwa na wakulima ili yachavushe mimea kama alizeti, machungwa, maharage, mabohora/mapesheni na
mahindi.
Katika nchi zilizoendelea
katika mifumo yao ya kilimo kama Marekani hutumia nyuki katika ushavushaji na
huku mazao wanayopata yakiwa na thamani ya mara kumi ya
thamani ya asali na nta.
Gladness anasema kwamba
uanzishaji na uendelezaji wa Hifadhi za Nyuki kwa ajili ya utalii ikolojia na
uhifadhi wa makundi ya nyuki, pamoja na mimea ya chakula chao na maabara za
kupima viwango vya mazao ya Nyuki
Wawekezaji, wahisani, taasisi na mashirika mbalimbali wanahamasishwa
kuwekeza katika kuanzisha maabara za kupima ubora wa asali na mazao mengine ya
nyuki ili kudhibiti viwango vya ubora wa mazao hayo.
Aidha anasema kwamba
ufugaji na uuzaji wa makundi ya nyuki hukamatwa na kuwekwa kwenye mzinga na
kisha kuuzwa kwa wafugaji wa nyuki, huku bei ya makundi ya nyuki wanaouma ni
kati ya shilingi 40,000 hadi 50,000 kutoka kwa mfugaji na wale wasiouma
wakifikia Sh. 50,000 hadi 70,000.
Biashara hii imeweza
kuwaongezea kipato wafugaji wengi hasa wale wanaouza makundi ya nyuki wasiouma,
hivyo kuweza kujimudu kimaisha na kusogeza mbele uchumi wa Taifa.
Uendelezaji wa sekta ya ufugaji nyuki utaleta
manufaa mengi wa kuongeza pato la Taifa, kuongeza ajira, na kipato kwa wananchi
kutokana na mazao ya nyuki na ya kilimo pia kuboresha mazingira.
Kwa mujibu wa Gladness, endapo kutakuwa na wafugaji 1,500,000 ambao
watajiajiri kwenye ufugaji nyuki na kuwa angalau na mizinga 50 kila mmoja,
mchango wa ufugaji nyuki unaweza kutambuliwa katika kuchangia na kupunguza
umasikini kwa uchumi wa nchi.
Wakarti mchango wa asali
ukiwa Sh. 1,250,000,000 kwa mwaka, mchanago w anta kwa wafugaji wa nyuki
kinafikia 371,250,000; sawa na USD 247.50, hivyo basi jumla ya kipato cha
mfugaji kwa mwaka kutokana na makundi 50 kikiwa Dola za Kimarekani 1,747.50.
“Tungeweza kuongeza kiasi
cha asali tunachouza nchi za nje cha tani 379 za nta na tani 275 za asali
kuwa tani 4,560 za nta zenye thamani ya Dola 15, 960, 000 na
tani 6,600 za asali zenye thamani ya Dola 9, 900, 000, Taifa
linaweza kupata kiasi cha Dola 25,860,000 kutokana na mauzo ya mazao ya
nyuki nje ya nchi na kukuza uchumi wetu.
Changamoto tuliyonayo ni udhibiti wa
ubora wa mazao ya nyuki na uzalishaji wa kibiashara, huku tukiwaomba Watanzania
wajikite kwenye sekta hiyo ya ufugaji nyuki kwa faida yao pia,” alisema Gladness.
kambimbwana@yahoo.com
No comments:
Post a Comment