BY KAMBI MBWANA
NATUMIA
fursa hii kukushukuru wewe ambaye umekuwa bega kwa bega tangu kuanzishwa kwa
blog hii ya Handeni Kwetu. Ingawa blog hii ilianzishwa rasmi mwaka jana
mwishoni, lakini ilinichukua miezi takribani 10 kuitendea haki.
Kwanini
nasema hivyo? Kutokana na kubanwa na majukumu mengine, iliniwia vigumu kuingiza
kazi mbalimbali kwa ajili ya kuwapa uhondo wasomaji wangu, ambao licha ya
changamoto hizo lakini walikuwa na mimi.
Wakati nausubiria mwaka mpya
Mpenzi
msomaji, najiona kuwa ni mwenye bahati sana. Kwani katika kipindi cha wiki ya
mwisho ya mwezi Desemba, tumeweza kuingiza wasomaji wapya zaidi ya 4000, kiasi ambacho
ni kikubwa mno katika blog inayochipukia.
Naamimi
wingi huo unatokana na kufanya kazi kwa moyo nikiwa na melengo zaidi ya kupeana
habari mbalimbali. Ndugu msomaji wangu, napenda kutangaza kuwa blog hii
haichagui.
Nimekuwa
mwepesi kuandika kila ninachoweza. Na kuanzishwa kwa blog hii kumetokana na
kuwa na malengo mawili makuu. Lengo la kwanza ni kutafuta mahali kwa kusemea,
nikiona kuwa kazi ya uandishi wa habari, nipo kwenye vyombo vya watu vya
habari.
Hivyo
kama wakati mwingine naweza kubanwa na sera ya kampuni, ingawa changamoto hizo
sijakutana nazo hadi muda huu, basi blog ya ‘Handeni Kwetu’ itanipa nafasi ya
kusema kila ninachojisikia ili mradi tu nisivunje sheria za Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania na kuzungumza na wasomaji wetu na ujumbe wangu kufika kwa wakati.
Lengo la
pili ni kutafuta namna gani naweza kuwaunganisha Watanzania wanaoishi ndani na
nje ya nchi, bila kusahau wakazi na wananchi wa wilaya ya Handeni yenye
changamoto nyingi.
Nashukuru
kwa dhati. Nashukuru maana nimepata mwangaza kugundua kuwa kazi zangu
zinapendwa. Na ndio maana nimekuwa mwepesi kuandika makala za aina mbalimbali,
ikiwamo kolamu ya ‘Mgodi Unaotembea’, ‘Mambo Fulani Muhimu’, ‘Siwezi Kuvumilia’
na zote ninazoandika katika uwepo wa kazi yangu ya uandishi wa habari na
uchambuzi wa makala zangu ambazo pia hupatikana katika gazeti la Mtanzania,
linalochapishwa na Kampuni ya New Habari 2006 Ltd, yenye maskani yake jijini
Dar es Salaam Tanzania.
Habari za
aina mbalimbali za michezo, siasa, afya, burudani na sanaa kwa ujumla, bila
kusahau biashara, afya na nyinginezo. Katika kulisema hilo, napenda kusema
mwaka mpya wa 2013 nitakuwa makini zaidi.
Nitafanya
kazi kwa moyo wote. Wewe kama mdau wa ‘Handeni Kwetu’, usisite kunishauri na
kunikosoa kwa njia mbalimbali, ikiwapo safu iliyoandikwa TOA MAONI YAKO KUHUSU
HANDENI KWETU.
Kwakuwa
sisi ni marafiki na ndugu moja, usisite pia kunitumia habari yoyote, picha
unayoona inafaa kuonwa kwenye blog ya ‘Handeni Kwetu’ ili iwe elimu kwa
wasomaji wote.
Napenda
kumaliza kwa kumshukuru tena Mungu pamoja na wewe kwa kuniunga mkono katika
kipindi chote cha mwaka 2012 na mwaka mpya wa 2013, huku nikiamini kuwa
tutaendelea kuwa pamoja wakati wote.
Asanteni
sana na tuendelee kushirikiana.
No comments:
Post a Comment