Na Kambi
Mbwana, Dar es Salaam
SHIRIKISHO
la Ngumi la Kimataifa (IBF) katika bara la Afrika, Ghuba ya Uajemi na Mashariki
ya Kati limemtamngaza Lucas Rutainurwa wa Kampuni ya Kitwe General Traders ya
jijini Dar es Salaam kama Promota wa mwaka 2012.
Akitangaza
uamuzi huo, Rais wa shirikisho hilo, Onesmo Ngowi, alisema Ruinurwa alifanikisha Watanzania
wawili kuwa mabingwa wa IBF katika bara la Afrika, Ghuba ya Uajemi na Mashariki
ya Kati.
Katika harakati zake za kuipa Tanzania sura ya
kimataifa katika tasnia ya ngumi za kulipwa Rutainurwa na kampuni yake ya Kitwe
General Traders waliandaa mapambano makubwa mawili ambayo yalizidi maandalizi
ya mapambano yote yaliyowahi kufanyika Tanzania kwa miaka ya karibuni.
Mwezi April mwaka 2012, Rutainurwa na Kitwe General
Traders waliandaa pambano lililowakutanisha mabondia Francis Cheka na Mada
Maugo wote wa Tanzania kugombea mkanda wa IBF bara la Afrika, Ghuba ya Uajemi
na Mashariki ya Kati katika ukumbi wa PTA jijini Dar-Es-Salaam. Katika mpambano
huo bondia Francis Cheka aliibuka kidedea baada ya kumsimamisha Maugo katika
raundi ya nane.
Francis
Cheka alitetea vyema mkanda wake huo tarehe 26 Desemba jijini Arusha
alishinda kwwa points bondia Chimwemwe Chiotcha kutoka
nchini Malawi katika pambano lao la raundi 12.
Mwezi wa
nane mwaka 2012, Rutainurwa na Kitwe General Traders waliandaa mpambano
mwingine kati ya bondia Ramadhani Shauri wa Tanzania na Sunday Kizito kutoka
Uganda kugombea mkanda wa IBF katika bara la Afrika.
Katika
mpambano huo bondia Ramadhani Shauri wa Tanzania alimsimamisha Sunday Kizito
kutoka Uganda katika raundi ya 9 na kutangazwa kuwa bingwa mpya wa IBF.
Kupatikana
kwa mabingwa hao, kumeifanya Tanzania kuwa nyumbani kwa mabingwa wawili wa IBF
na hivyo kuiweka nchi hii katika ngazi moja na chache duniani hususa katika
bara la Afrika zikiwemo Afrika ya Kusini, Ghana, Morocco, Algeria na
Cameron.
No comments:
Post a Comment