Mkurugenzi wa Grace Product, Elizabeth Kilili akiwa ofisini kwake.
Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
MKURUGENZI wa Kampuni ya Grace
Product Ltd, ya jijini Dar es Salaam, Elizabeth Kilili, amesema kwamba Watanzania
wengi wana magonjwa ya ngozi na kuhatarisha afya zao.
Elizabeth ameyasema hayo muda
mfupi alipokuwa akizungumza na Handeni Kwetu ilipotembelea ofisini kwake, Ukonga na kuonyesha bidhaa
zake zinazopambana na magonjwa ya ngozi.
Akizungumzia hali hiyo,
Elizabeth alisema kwamba kutokana na hilo, bidhaa zake zinaweza kuondosha
kabisa magonjwa hayo, yakiwamo mapunye, mba, muwasho na yote yanayosababisha
ngozi zishindwe kuwa kwenye mwonekano mzuri.
Alisema bidhaa zake kama vile
Shampoo, loation na sabuni yake inayojulikana kama Grace Manjano Soap
zinazopatikana madukani kote ni nzuri kiasi cha kuondoa matatizo hayo.
“Watanzania wengi wana
matatizo ya ngozi kutokana na mazingira au shughuli zetu pamoja na wengineo
kuathiriwa zaidi na bidhaa walizowahi kutumia.
“Kwasababu hiyo, bidhaa zangu
zote ambazo kwa sasa zipo sokoni zinba uwezo wa kuondoa matatizo hayo na
kuwafanya watu wawe kwenye afya njema,“ alisema.
Kwa mujibu wa Elizabeth,
bidhaa zake nyingine anazotengeneza ni pamoja na sabuni ya kufulia na kuoshea
vyombo inayoitwa liquid Soap, Disinfectant inayotumika kusafisha nyumba na
choo.
No comments:
Post a Comment