Tafuta
muda wa mapumziko na mwenzako
Faragha ya wawili wapendanao hawa
Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
KUNA watu ambao licha ya kuwa na
uwezo na muda wa kuweza kutoka pamoja na wapenzi wao, ila jambo hilo ni gumu
zaidi kwao.
Wapo nyumba ile ile, eneo lile lile.
Hata muda wa kutoka nje ya maeneo ya nyumba zao kwa ajili ya kuzungumza hili na
lile na wake au waume zao hawana.
Hili nim tatizo kubwa. Ni tatizo,
hasa pale mwanaume au mwanamke anapoamua kutoka peke yake au kutoka na watu wa
nje.
Kwanini? Najua kuna wakati mtu
anatamani kuwa peke yake, ila katika suala zima la mapenzi, kunaashiria kwamba
uhusiano wao umeanza kuyumba.
Unatakiwa wewe na mtu wako kuongeza
mapenzi kila wakati kama njia ya kudumisha uhusiano wenu au ndoa zenu kwa nyie
mliofunga ndoa.
Huo ndio ukweli wa mambo. Jaribu
kumchukua mpenzi wako na kumpeleka nje ya eneo mlilozoea siku zote. Mfano, kama
unaishi Sinza, jijini Dar es Salaam, basi mkapumzike Kawe, Msasani katika beach
yoyote ambayo ni chaguo lenu.
Huo sio utaratibu wa wageni.
Kutembea na kufurahia sio utamaduni wa Wazungu kama wanavyofanya baadhi yao.
Hapo hujaiga.
Na hata kama utakuwa umeiga
utaratibu huo, hakika hujaiga tabia mbaya zisizofaa katika jamii, hasa kama
umeangalia na kipato chako.
Kwa mfano, ukienda beach ya
kulingana na kipato chako, au ile ya Coco Beach ambayo kila Mtanzania anaweza
kwenda hapo bila malipo ni jambo zuri na linaloweza kuongeza ladha ya uhusiano
wenu.
Hapo mkifika mtakaa pamoja naa
kuzungumzia mustakabali wa mapenzi yenu. Mtaangalia yalipotoka na yanapokwenda.
Kama mlikwazana katika kipindi cha
nyuma, hakika mtajua kosa lenu na kujisahihisha kwa nia ya kufanya marekebisho
mazuri kwa ajili ya penzi lenu.
Na kama mna kipato kizuru, basi
mnaweza kwenda katika hoteli zenye beach nzuri na zenye ulinzi wa kutosha.
Sitaki kuzitaja, maana zipo nyingi zenye hadhi ya kuvutia.
Hapo penzi litazidi kuchanua.
Mtakuwa pamoja na kuangalia kila linalopita mbele yenu, iwe baya au zuri. Hapo
kila mmoja atatoa msimamo wake na namna gani mnaweza kusonga mbele zaidi.
Kwanini uende katika maeneo hayo
wakati unapoanza penzi jipya huku ukishindwa kwenda tena mnapokuwa pamoja?
Nadhani kuna kila sababu ya
kujiangalia upya, kama tuna lengo la kutoa dosari kwenye uhusiano wenu, maana
mapenzi yana utamu wake.
Mwambie mpenzi wako. “Leo najisikia
kuzungumza na wewe nje ya nyumba yetu”.
Nadhani naye atajisikia faraja kama
bado anapendwa na kuthaminiwa, ukizingatia kwamba wapo wanaowafanya wake zao ni
walinzi wa nyumba huku wao wakila ‘bata’ kustarehe na wapenzi wa pembeni au
marafiki zao.
Tuache tabia hiyo ya ajabu na
isiyokuwa na mashiko katika jamii, ukizingatia kwamba mapenzi ni mazuri kama
yakihusisha wawili wapenda nao.
Tukutane wiki ijayo.
0712 053949
0753 806087
No comments:
Post a Comment