Rais wa TFF, Leodgar Tenga
Na
Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
RAIS wa
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania
(TFF), Leodegar Tenga amewashukuru wajumbe wa Mkutano Mkuu kwa kupigia kura
waraka wa marekebisho ya Katiba, kwakuwa wametimiza wajibu wao.
Akizungumza
na Waandishi wa Habari, Dar es Salaam
leo, Rais Tenga amesema marekebisho ya Katiba ni jambo muhimu, lakini lazima
yapate ridhaa ya wanaohusika ambao ni wajumbe.
“Nawasukuru wajumbe kwa kupitisha jambo
hili. Nawashukuru wote, waliokubali na waliokataa. Ndivyo demokrasia ilivyo.
Tulitaka waseme ndiyo au hapana, hivyo tulitarajia kupata majibu yoyote kati ya
hayo mawili.
“Marekebisho
mengine yalikuwa ni maelekezo (directives) kutoka FIFA na CAF. Katiba yetu
inasema tutatekeleza maagizo ya CAF na FIFA, lakini kwa misingi ya utawala bora
tuliona ni lazima tupate ridhaa kutoka kwa wajumbe,” amesema.
Jumla
ya wajumbe waliopiga kura kwa njia hiyo ya waraka ni 103 ambapo 70 waliunga
mkono wakati waliokataa ni 33. Idadi hiyo ni asilimia 68 ya kura zote zilizopigwa,
hivyo kupatikana theluthi mbili ya kura zilizopigwa ili kufanya marekebisho
kikatiba.
Vipengele
vilivyoingizwa katika marekebisho hayo ni ‘club licencing’ kama ilivyoagizwa na
Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF), Kamati ya Rufani ya Uchaguzi wa TFF
kama ilivyoshauriwa na Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) na
kuondoa nafasi ya Makamu wa Pili wa Rais.
Vilevile
Kamati ya Utendaji itakutana Desemba 23 mwaka huu kufanya marekebisho ya Kanuni
za Uchaguzi, kutokana na kupitishwa kwa marekebisho hayo ambayo yanaunda Kamati
ya Rufani ya Uchaguzi wa TFF. Pia itachagua wajumbe wa Kamati ya Rufani ya TFF.
Mkutano
Mkuu wa TFF ambapo pia utakuwa na ajenda ya uchaguzi utafanyika Februari 23 na
24 mwakani. Kwa mujibu wa Katiba ya TFF, wajumbe wanatakiwa kupewa taarifa ya
Mkutano Mkuu kabla ya siku 60.
No comments:
Post a Comment