Meya wa Arusha, Gaudence Lyimo
Na Mwandishi Wetu, Arusha
JIJI la Arusha linazidi kubarikiwa baada ya kuteuliwa kuwa Makao Makuu
ya Chama cha Ngumi za Kulipwa Cha Afrika ya Mashariki na Kati (ECAPBA), huku
muombaji mkuu wa jambo hilo akiwa ni Mstahiki Meya wa Arusha, Gaudence Lyimo,
akiwa na lengo la chama hicho kuwa karibu na Jumuiya ya Afrika ya Mashariki (EAC).
Rais wa ECAPBA, Onesmo Ngowi
Akizungumzia suala hilo, Rais wa
ECAPBA Onesmo Ngowi, alimhakikishia meya kuwa ECAPBA itahamishia makao yake
makuu katika jiji la Arusha, ikitoka katika Halmashauri ya Manispaa ya Moshi.
Alisema kuwa Juhudi za Lyimo za
kukuza michezo na kukuza utalii katika jiji la Arusha ni moja ya sababu
zilizomfanya rais wa ECAPBA kuamua kuhamishia ofisi hizo katika jiji la Arusha.
“Uamuzi huo uliungwa mkono na
mmoja wa wanachama wa ECAPBA bw. Daudi Chikwanje ambaye ndiye Katibu Mkuu
wa Chama Cha Ngumi za Kulipwa Cha Malawi.
“Nchi ya Malawi ni mwanachama wa
ECAPBA pamoja na Kenya, Zambia, Ethiopia, Burundi, Sudan ya Kusini, DRC,
Rwanda, Uganda na Sudan,” alisema.
ECAPBA inaratibu ubingwa unaojulikana
kama ECAPBF ambao unawapa mabondia wa ukanda huu kuwa mabingwa imara wa ngumi
Afrika.
No comments:
Post a Comment