Wema Sepetu ndio huyu sasa
Na Mdakuzi wetu
Licha ya kuandikwa sana
katika vyombo vya habari na wakati mwingine habari mbaya kwake, lakini msanii
wa filamu na mrembo wa zamani wa Miss Tanzania, Wema Sepetu, ameonekana
kuwa na mvuto unaochanganya wengi.
Wema ambaye kwa sasa wanaendeleza uhusiano wake na Diamond
kwa siri kubwa, sura yake inauza kiasi cha kuwafanya waandishi wamsake kila
wakati, huku wasanii na watu wengine kutaka ukaribu nae.
Silaha ya Wema magazeti
Uchunguzi uliofanywa na Handeni Kwetu, umegundua kwamba kati
ya watu waliokuwa kwenye uhusiano na mwanadada huyo, wamefanikiwa kujenga
majina yao na
kufanya vyema katikaa kazi zao.
Miongoni mwa watu hao ni Fresh Jumbe, Chalz Baba, Steven
Kanumba, Diamond ambao ingawa walikuwa wakijulikana, lakini umahiri na majina
yao yalizidi kuchanua katika uhusiano na malkia huyo.
Jambo hilo
lilisababisha watengenezaji wa bia ya Serengeti, wabuni wazo la wasanii wa
filamu akiwamo Ray, Wema, Steve Nyerere na JB wazunguuke katika mikoa
mbalimbali katika shoo ya Fiesta.
Katika mikoa yote, Wema alionekana kunogesha zaidi shoo
hizo, huku akiacha watu wakiwa kwenye pilika pilika nyingi, wakionekana
kupagawa juu ya haiba na mwonekano wa mrembo huyo wa zamani wa Tanzania.
Mashabiki wa filamu na muziki watambuka shoo ya mjini Dodoma, pale Wema
alipoonekana jukwaa moja na Diamond, jambo ambalo lilizidi kumng’arisha kijana
huyo aliyekulia maeneo ya Tandalee.
Kwa sababu hiyo, kuna kila sababu ya kusema kuwa mvuto wa
Wemaa ni mkubwa kiasi cha kuweza kumpa umaarufu mtu yoyote atakayeweza kuwa na
uhusiano na malkia huyo anayemng’aa kwa miaka kadhaa sasa.
Huyo ndiye Wema Sepetu
No comments:
Post a Comment