Heri ya Krismasi
Na Timu ya Handeni Kwetu
LEO
Tanzania na Dunia nzima kwa ujumla inaadhimisha Sikukuu ya Krismasi, ikiwa ni
kumbukumbu ya kuzaliwa Yesu Kristo. Kwa sababu hiyo basi, Handeni Kwetu inachukua fursa hii
kuwatakia Wakristo wote duniani sikukuu njema.
Handeni
Kwetu tunaomba msheherekee kwa amani Sikukuu hii pamoja na kukumbuka walau
mstari mmoja wa kwenye kitabu Kitukufu cha Biblia iwe kama
faida kwenu kwa siku ya leo duniani.
Pia
muitumie Sikukuu hii kuwaombea wengine wenye matatizo ili Mungu awape furaha na
amani mioyoni mwao. Zile nchi zenye vurugu za kidini basi kadhia zao hizo
zikome kutokana na dua zinazoelekezwa kwao.
Yale
mataifa makubwa yaliyoendelea kiuchumi yazidi kuzikumbuka nchi masikini kwa
kuwapa mikopo isiyokuwa na masharti magumu yanayosababisha kuvunja uaminifu wa
pande zote mbili.
Kwa
kuyasema hayo, tunaamini leo ni siku nzuri kwa watu wote, huku ikiwa bado siku
tano tu mwaka huu kumalizika na kuingia 2013 kama uhai baaadhi yao tutakuwa nao.
Asanteni sana kwa kuinga mkono
blog hii ya Handeni Kwetu, huku tukiamini kuwa tutaendelea kuwa bega bega kwa bega
na nyie kwa kuwaletea habari mbalimbali pamoja na makala zilizoandikwa kwa
kina, ikiwamo siasa, michezo na nyinginezo.
+255 712 053949
+255 753
806087
No comments:
Post a Comment