Mhariri Mtendaji wa New Habari 2006 Ltd, Absalom Kibanda
Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
MHARIRI Mtendaji wa
zamani wa Kampuni ya Free Media Ltd, inayochapisha gazeti la Tanzania Daima, Absalom
Kibanda, leo ametangazwa rasmi kuwa Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya New Habari
2006 Ltd.
Kibanda sasa anakuwa
bosi wa waandishi wote katika kampuni hiyo inayochapisha magazeti ya Mtanzania,
Rai, Dimba, Bingwa na The African, iliyokuwa chini ya Mkurugenzi wake, Hussein
Bashe.
Ofisa Mtendaji Mkuu, New Habari 2006 Ltd, Hussein Bashe
Akizungumzia ujio wake
kwenye kampuni hiyo, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Hussein Bashe,
alisema Kibanda sasa ni mwenzao kwa ajili ya kuitumikia New Habari 2006 Ltd.
“Kuanzia leo tutakuwa
pamoja na mwenzetu Kibanda katika kampuni hii na kushirikiana naye kiutendaji
na majukumu yake,” alisema Bashe.
Naye Kibanda alisema alisema
haoni sababu kwanini kampuni hiyo isipige hatua, hasa kutokana na rasirimali
watu zilivyokuwa za kutosha.
Alisema kwa sababu
hiyo, atashirikiana kwa karibu na wafanyakazi wote kwa ajili ya kusonga mbele
na kuwa chumba cha habari chenye mafanikio makubwa nchini.
“Nashukuru sana, huku nikiamini kuwa
tuliokuwa upande wa habari tunajua kwa dhati wakiwamo wahariri tunaokutana nao
mara kwa mara kwenye shughuli zetu,” alisema Kibanda.
Kwa mujibu wa Kibanda,
alikuwapo katika kampuni hiyo miaka 12 iliyopita wakati huo ikijulikana kama Habari Corporation.
No comments:
Post a Comment