Ofisa Habari wa TFF, Boniface Wambura
Na Mwandishi Maalumu, Dar es Salaam
MECHI ya kirafiki ya Kimataifa
kati ya Tanzania (Taifa
Stars) na Zambia
(Chipolopolo) lililochezwa Desemba 22 mwaka huu, imeingiza Shilingi milioni 109,197,000.
Akizungumza jijini Dar es Salaam,
Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka nchini (TFF), Boniface Wambura, alisema fedha
hizo zimepatikana kutokana na watazamaji 17,383 waliokata tiketi kushuhudia
mechi kwa kiingilio cha sh. 5,000, sh. 7,000, sh. 10,000, sh. 20,000 na sh.
30,000.
Mgawanyo wa mapato hayo ulikuwa kama ifuatavyo; asilimia 18 ya Kodi ya Ongezeko la
Thamani (VAT) ni sh. 16,657,169.49, maandalizi ya mchezo sh. 55,339,510, tiketi
sh. 5,803,900, ulinzi na usafi kwa Uwanja wa Taifa sh. 2,350,000, Wachina
(technical support) sh. 2,000,000, umeme sh. 300,000 na maandalizi ya uwanja
(pitch marking) sh. 400,000.
Nyingine ni bonasi kwa Taifa Stars
sh. 13,826,313, asilimia 20 ya gharama za mchezo sh. 2,504,022, asilimia 10 ya
uwanja sh. 1,252,011, asilimia 5 ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF)
sh. 626,005 na asilimia 65 ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) sh.
8,138,070.
Mapato ya mechi nyingine za Taifa
Stars ilizocheza nyumbani mwaka huu yalikuwa Taifa Stars vs Jamhuri ya
Kidemokrasi ya Congo-DRC (Leopards) iliyofanyika Februari 23 mwaka huu Uwanja
wa Taifa, Dar es Salaam
sh. 32,229,000. Taifa Stars vs Msumbiji (Mambas) iliyochezwa Februari 29 mwaka
huu sh. 64,714,000.
Taifa Stars vs Malawi (The Flames) iliyochezwa Mei 26 mwaka huu
Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam
iliingiza sh. 40,980,000.
Taifa Stars vs Gambia (The Scorpions) iliyochezwa Juni 10 mwaka
huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam zilipatikana
sh. 124,038,000 na Taifa Stars vs Kenya (Harambee Stars) iliyofanyika
Novemba 14 mwaka huu Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza iliingiza sh. milioni
45.
Katika hatua nyingine, Kamati ya Utendaji ya Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), imemteua Idd Mtiginjola kuwa Mwenyekiti wa
Kamati ya Rufani ya Uchaguzi ya TFF iliyoundwa kutokana na marekebisho ya
Katiba yaliyofanyika hivi karibuni.
Mtiginjola ambaye ni Wakili wa
kujitegemea ataongoza kamati hiyo yenye wajumbe watano ambayo sasa itakuwa
chombo cha mwisho kusikiliza rufani zinazotokana na uchaguzi wa TFF, na
wanachama wa TFF ambao hawatakubaliana na uamuzi wa Kamati ya Uchaguzi ya TFF.
Kabla ya uteuzi huo, Mtiginjola
alikuwa mjumbe wa Kamati ya Nidhamu ya TFF inayoongozwa na Kamishna wa Polisi (CP)
mstaafu Alfred Tibaigana. Nafasi yake katika kamati hiyo na ile ya mjumbe
mwingine Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Shabani Semlangwa aliyefariki dunia
Julai mwaka huu zitajazwa hivi karibuni.
No comments:
Post a Comment