Huyu ni Mr Nice, mkali aliyetokelezea sana kabla ya kutoweka katika 'game'
ALITOKELEZEA
Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
MWIMBAJI na mfalme wa
muziki wa Takeu aliyousisi kwa Tanzania,
Nice Lucas Mkenda maarufu kama Mr Nice ni
miongoni mwa wasanii waliowahi kuvuma mno miaka ya nyuma. Kila mmoja alikuwa
akipenda kumuona nyota huyo.
Nyimbo alizowahi kutoa
msanii huyo ni pamoja na Mama, Kikulacho, Rafiki, Fagilia na nyinginezo ambazo
hakika watu walizipenda na kuziheshimu.
Sio Tanzania tu, bali nchi nyingi za
Afrika Mashariki na Kati, Nice alipendwa na kukubalika mno.
Nakumbuka, Nice ilibaki
kidogo aonekane kama Rais, kwani nchini Msumbiji, visiwa vya Comoro, Uganda,
Kenya, Rwanda jina lake lilivuma na wadau wengi walisema kumbi za kufanya shoo
jamaa huyo zilikuwa chache, huku viwanja vya wazi ndio ilikuwa mahali pake.
Huyu Mr Nice alivuma balaa
Watoto mtaani walikuwa
wakicheza au kunyoa kama Mr Nice, hasa ile
style yake ya kunyoa unga unga na kupaka rangi nyeusi na kutelezesha mstari
sehemu ya sikio na kuonekana nadhifu.
Kuvuka kwake kulizidi hasa
alipokuwa akiingia kwenye ugomvi na kupigwa mara kwa mara na nyota mwenzake,
Godfrey Tumaini, maarufu kama Dudu Baya, a.k.a
Zeze Dudu.
Wengi walimlilia sana waliposikia anaonewa
ovyo na Dudu Baya. Pamoja na sifa zote hizo, heshima yote hiyo, lakini hali ni
mbaya. Jamaa huyo hasikiki tena jukwaani.
Imefikia wakati mwaka
unakwisha bila kuonekana jukwaani. Katikati ya mwaka huu alionekana kwenye shoo
ya Fiesta ya mjini Moshi, watu wakasema jamaa anataka kurudi tena?
Kwanini? Uwezo wake
umeisha? Anaishi vipi? Wadau wa burudani tunakutana naye katika baadhi ya kumbi
za starehe akipata moja moto moja baridi, hasa kwa wale wanaoendelea kumheshimu
kumpa ofa.
Sasa basi, kama wewe ni swahiba wake, ndugu yake, Handeni Kwetu
inataka kujua sanaa yake imeishaje? Mwambie kuwa tumemkumbuka sana. Mwambie aone nyota wapya wanavyovuna
fedha kupita kiasi.
Hivi unajua kuwa kama leo hii Mr Nice angekuwa Diamond, Ommy Dimpozi sijui
angeitwa nani. Majina yote yangekuwa yake, hasa yale Fremason kama
wanavyozushiwa wengine.
Nakusalimia bwana Mr Nice kama kweli uwezo unao tukutane jukwaani kwa nyimbo nzuri
na zitakazorudisha heshima yako, vinginevyo tutaendelea kusema kuliwahi kuwa na
Mr Nice.
0712 053949
0753 806087
No comments:
Post a Comment