Wadau wakiangalia vitalu vya miti
Fresh Farms & Tours (T),
biashara tanzu ya Anesa Co.Ltd (Nyaluke Business Empire); inajishughulisha na
upandaji, utunzaji na uendelezaji wa mashamba ya miti ya mbao, karatasi na
nguzo-mkoani Iringa.
Vilevile inahusika na uvunaji na
usambazaji wa mazao ya miti, (mbao na nguzo za umeme) sambamba na ufugaji.
Fresh Farms ilianzisha programu
maalumu, mapema mwaka jana; inayolenga kuwawezesha watanzania wengine kuwekeza
katika kilimo cha miti kwa urahisi.
Tayari makumi ya watanzania
wamechangamkia fursa hii. Fresh Farms & Tours (T) tunapenda kuwaarifu wale
wote wenye nia ya kuwekeza nasi, kuwa kuanzia Februari Mosi, 2013 kutakuwa na mabadiliko
ya bei na gharama za uendeshaji kwa mashamba ya miti.
Mashamba tunayoyauza laki sita
kwa sasa; bei mpya itakuwa milioni moja; na yale tunayouza laki nane gharama
yake itakuwa milioni moja na nusu.
Bei hizi hazitawaathiri wateja wa
awali na wale ambao wamekwisha wasilisha oda zao. Fresh Farms & Tours (T)
tunaendelea kuboresha huduma, taarifa na usaidizi kwa wote wanaowekeza nasi.
Fresh Farms & Tours (T)
tunakutakia heri ya Mwaka mpya wa 2013 na tunakukumbusha ile salamu
yetu(motto); "Greening the world and Feeding People".
IMETOLEWA NA:
Albert Nyaluke Sanga, (SmartMind)
Mtendaji Mkuu-Fresh Farms & Tours(T),
(C) 2012
No comments:
Post a Comment