https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543


Recent Post

Thursday, December 06, 2012

GIDABUDAYI AENDELEA KUWASAKAMA GULAM NA BAYI

ZIKIWA zimesalia siku mbili tu, uchaguzi wa kamati ya olimpiki (TOC), ufanyike mjini Dodoma, Mwanariadha wa zamani aliyepata kupeperusha vema bendera ya taifa katika miaka ya 90, Wilhelm Gidabuday, ameendelea kuusakama uongozi wa TOC unaomaliza muda wake, safari hii akiwataka kuheshimu maadili ya Baba wa Taifa na kuachia madaraka.
Gidabuday aliyasema hayo alipozungumza na KIJIWE CHETU kwa njia ya Simu na kuutaka uongozi huo uliochini wa mwenyekiti Gulam Rashid na Katibu wake, Filbert Bayi kuiga kitendo cha kiungwana uliooneshwa na Marehemu Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere wa kuachia madaraka katika kipindi ambapo  watanzania walimuhitaji.
Alisema viongozi hao hawana budi kuachia watu wengine waliona na machungu na TOC kuongoza ili nchi hii iweze kufikia malengo yake na hatimaye kupata mafanikio katika michezo kama ilivyokuwa katika kile kipindi walipokuwa wanakimbia.
“Naomba kwa heshima ya mchezo wa riadha, kwa heshima yao kama wakongwe na mashujaa wa Taifa letu katika Riadha, Gulam na Bayi waone umuhimu wa kuachia madaraka kwa wengine kama alivyofanya Marehemu Baba wa Taifa kama njia ya kutunza heshima zao kitaifa na kimataifa,” alisema Gidabuday
Alisema pamoja na kusalia siku chache uchaguzi ufanyike, fursa ya kufanya maamuzi ya kiungwana bado ipo na kuwataka kufanya hivyo ikiwa kweli tuhuma za ubadhirifu na ufisadi ambayo imekuwa ikielekezwa kwao si kweli, akisisitiza kuwa hata hivyo kutokana na Viongozi wanaomaliza muda wao ndani ya TOC kutegemea ofisi hiyo ni vigumu hilo kutokea.
“Ikiwa kweli hawa viongozi wanadai kwamba tuhuma dhidi yao si kweli basi walithibitishe kwa kuachia uongozi kwa watu wengine, ila naamini hilo haliwezakani, naomba ninukuu kifungu cha maadili ya IOC (code of ethics), ambayo wao wameivunja wazi wazi na wanafanya hivyo kwa sababu maisha yao yanategemea ofisi ya TOC kwa gharama ya wanariadha wetu na serikali yetu,” alisema.
Akizungumzia madai yaliyotolewa dhidi yake kwamba yeye anachuki binafsi na mmoja kati ya Viongozi walioko madarakani, Gidabuday alisema yeye anazungumza ukweli, ukweli ambao kwa wengi wasiopenda maendeleo wanamuona kama msaliti na kusisitiza kuwa katika kitabu cha maadili ya IOC ambayo iko sambamba na Maadili ya TOC na jamhuri ya muungano wa Tanzania kila kitu kiko wazi.
Kuhusu swala Kambi ya timu ya Taifa ya vijana iliyoenda na kufanya utumbo katika michezo ya olimpiki ya mwaka huu jijini London, Uingreza na madai ya TOC kwamba wao hawahusiki na maandalizi ya kikosi, Gidabuday alisema huo ni upotoshaji wa katiba ya TOC na IOC, kwani jukumu la kuandaa wanamichezo liko chini ya TOC kwa mujibu wa katiba na kitabu cha Maadili ya IOC.
“Kipengele cha saba katika kitabu cha maadili, kinasema ni kamati ya Olimpiki inawajibika kuandaa wakimbiaji, kuwatunza kiafya, na kuwahudumia kabla na baada ya Safari hadi mwisho wa michezo sasa iweje wao waseme hawahusiki kuandaa kikosi na kama hawahusiki ile kambi waliyoiweka Kibaha ilikuwa inakazi gani,” alihoji Gidabuday.

Uchaguzi wa kamati ya olimpiki unatarajiwa kufanyika Desemba 8 mjini Dodoma chini ya uangallizi wa Mwenyekiti wa kamati ya Uchaguzi na aliyekuwa mwenyekiti wa zamani wa timu ya Yanga, Lyoid Nchunga.


Bayi na Gulam hawana hata chembe ya hekima (Wisdom): 
Naomba kunukuu MAADILI (CODE OF ETHICS) za IOC wao wamezivunja wazi wazi na kwa vile inaonyesha wazi wazi kwamba maisha yao yanategemea ofisi ya TOC wapo tayari kufanya lolote ili warudi, wale na waishi vizuri kwa mika mingine minne; wakidhani serikali haina mkono mrefu wala jicho lionalo mbali!!.
1). Kwa mujibu wa kitabu cha SPORTS ADMINISTRATION MANUAL lililochapishwa na Olympic Solidrity chini ya uangalizi wa INTERNATIONAL OLYMPIC COMMITTEE toleo la 2010; kuna mambo matatu ambayo mimi ninaona wazi kwamba waheshimiwa hao wamekiuka maadili ya IOC ambayo ni sambamba na maadili ya JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA:
  (A). Dignity: Kuna vipengele sita ambavyo mimi naona vyote vimekiukwa, lakini kipengele cha 6 ambacho kinasema; 
7. The Olympic parties shall guarantee the athletes conditions of safety, well-being and medical
care favourable to their physical and mental equilibrium.
Ninathibitisha kipengele hicho maana HAPAKUWA NA DOCTOR KTK KAMBI ILIYOWEKWA KWENYE HOSTEL YA KATIBU MKUU WA TOC!!. Ndo maana mwanariadha MUSANDUKI MUHAMED aliugua alipofika LONDON kwa kukosa matibabu ya awali ambayo angeyapata wakati akiwa mazoezini. 'Hili ni kosa ambalo limeelezewa kuwa ipo katika "read line which must not be breached"
   (B). Integrity: Kuna vipengele vitano pia, lakini twende katika kipengele cha 3  ambacho kinasema; 3. "Any form of conflict of interest must be avoided". 
Kipengele hicho kinajieleza vizuri na ushahidi wake ni wazi; KWAMBA, TIMU YA TAIFA LETU ILIPELEKWA NYUMBANI AMA KATIKA HOSTEL ZINAZOMILIKIWA NA KATIBU MKUU WA TOC, AMBAYE PIA NI MJUMBE WA KUDUMU WA CHAMA CHA RIADHA TANZANIA, HIVYO BASI KATIBU HUYO ALITUMIA INFLUENCE YAKE KUPATA MASILAHI YATOKANANAYO NA MASHINDANO YA OLYMPICS!!. KATAA KUBALI HILINI KOSA LA JINAI HATA HAPA KWETU, AMA KWA JINA LINGINE TUNAITA "ABUSE OF POWER". MATUMIZI MABAYA YA MADARAKA. PIA KATIBU HUYO MKUU ALIJILIPA MWENYEWE KWA KUJUA NI KIASI GANI KINATOLEWA KWA MAANDALIZI YA TIMU.  Pia ifahamike kwamba hakuna katibu mkuu mwingine duniani wa NATIONAL OLYMPIC COMMITTEE ya nchi zaidi ya 200 duniani zinazoshiriki Olympics amediriki kupeleka timu ya taifa lake katika himaya yake ili afaidike na mapato ya moja kwa moja kutoka Olympic Solidarity.
     (C). Resources: Katika section hiyo kuna vipengele vine lakini mimi niongelee vipengele  1 na 2 inayosema kwamba; 1. The Olympic resources of the Olympic parties may be used only for Olympic purposes.
2.1 The income and expenditure of the Olympic parties shall be recorded in their accounts,
which must be maintained in accordance with generally accepted accounting principles.
An independent auditor will check these accounts.
Nawatuhumu kivipi; kwa sababu: Tumekuwa tukilalamikia mapato na matumizi kutoka kwa Olympic Solidarity na dola 100,000 kutoka India, bila kusahau dola 100,000 ambazo zilitumika kwa maandalizi ya timu(kimsingi mzee alijilipa mwenyewe) fedha ambazo BAYI NA GULAMU wanakuwa bubu pindi wanapoulizwa, pia kuna uwezekano kwamba accountant anayekagua mapato na matumizi ya TOC ni mfanyakazi/mjumbe wa TOC!!. Sasa basi ipo wapi dhana ya IOC inayotaka kuwepo kwa INDEPENDENT AUDITOR ?.
NINI KINAFUATA BAADA YA HAYO YOTE:
A fall from grace, 'Ipo siku, tena hivi karibuni BAYI ataanguka kutoka juu!!, nikimaanisha siri zake zote zitakuwa hadharani na dunia nzima itajua, na tunafahamu kuwa mataifa ya mgharibi haipendi UFISADI, na FILBERT BAYI ana sifa nzuri sana kimataifa kwani anajulikana kama "The miracle miler", ila mimi nasema laiti angelijua jinsi ambavyo heshima yake itakavyoshuka kama ile ya LANCE AMSTRONG, asingekuwa na kiburi cha kuwa kin'gan'ganizi katika uongozi bali aachie madaraka ili aonekane wa maana hadi kufa kwake!!. AMA SIVYO tayari tumeandaa sahii 2,000 za wadau ambao dunia haitawadharau, na tutatuma malalamiko yetu hadi IOC na kopi kwa Olympic Solidarity, ripoti ambayo itaipaka matope serikali sababu kuna VIGOGO WAWILI wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo wamehusishwa na ripoti yetu ambayo gharama ya uchunguzi imechangiwa na wazalendo. Asishangae muda mfupi ujao akabatizwa jina la "The criminal Miler badala ya lile zuri la The miracle miler".
Yeye na hela yake SISI na uzalendo wetu na nchi yetu!!.
Mambo mengine yaliyoharibika BAYI na Gulamu walipoingia:
1). Olympic Possible ilifutwa, program ambayo ndio iliwawezesha wao kushinda medali 1980 baada ya kufadhiliwa kupitia program hiyo inayofadhiliwa na IOC kila mwaka. Je wamezi-locate hizo hela wapi?.
2). Matumizi mabaya ya PUMA na LINING ambapo hadi sasa taifa letu halina SPONSOR kutokana na Tanzania kuonekana matapeli sababu ya wawili hao ambao bora wafe kuliko kukosa uongozi TOC.
3). Zanzibar na Bara kutumiwa vibaya kwa madai "TOC INAJALI MUUNGANO", wakati huo ndo uongo wao, tangu waingie madarakani si Zanzibar wala Bara wamejengewa chochote, bali wao wamejijengea mashule, majumba ya kifahari na sasa wanaomba kura ili labda wakamilike kwa kujijengea AIRPORTS KABISA!!.
HII INASIKITISHA, INASHANGAZA, INAKATISHA TAMAA, LAITI BMT WANGETAMBUA HILO TANZANIA TUTASONGA MBELE!!.
By: Wilhelm F. Gidabuday.
NB: Niliyoyasema nimeyanukuu kutoka kwenye kitabu cha IOC, ukihitaji kopi za kurasa muhimu za kitabu hicho please be free to ask me at any time:

No comments:

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...