https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543


Recent Post

Thursday, December 06, 2012

FM ACADEMIA KUDONDOSHA "VUNDES STYLE" LEO AVENTURE MOSHI

Bendi ya muziki wa dansi ya FM Academia "Wazee wa Ngwasuma" inayoendelea kukonga nyoyo za wapenzi wa muziki wa dansi hapa nchini, wanatarajia kuwaburudisha mashabiki wake na wakazi wa mji wa Moshi LEO katika shoo kali na ya kukata na shoka katika ukumbi wa Aventure, ulioko Majengo, Moshi kuanzia Saa tatu usiku.

Akizungumza na Mtanzania kwa njia ya simu, Rais wa bendi ya Fm Academia, Nyosh El Saddat, alisema wanatarajia kuwapagawisha wakazi wa Moshi na viunga vyake katika usiku huo kwa kupiga Shoo kali pamoja na kuonesha staili mpya ya kucheza ya Vundes style na kuongeza kuwa wanatarajia kufanya shoo hiyo kuwa ya kipekee kuwahi kutokea katika mji wa Moshi.


"Tunakuja kuwapa sindano za moto, ni muda mrefu Fm Academia, wazee wa Ngwasuma hatujafika Moshi na Arusha, tutatumia usiku wa Academia, kushusha Ngwasuma za hatari, pia tutaonesha watu ya Moshi namna ya kucheza Vundes, pia tunataka kufanya shoo hii iwe ya kipekee kuwahi kutokea," alisema Nyosh El Saddat.


Nyoshi alisema katika kuhakikisha wanawaridhisha wapenzi wa Ngwasuma na kutoa zawadi ya krimasi kwa wapenzi wa muziki wa dansi katika mji wa Moshi, Fm Academia imejipanga kutoa burudani ya kufa mtu ambapo watapiga angalau nyimbo mbili kutoka katika albamu yao mpya ya Chuki ya Nini.


"FM Academia itapiga nyimbo mbili zilizoko katika albamu ya Chuki ya nini, kama zawadi ya krismasi kwa wapenzi wa muziki wetu, kujeni mucheze na Wazee wa Ngwasuma, tufunge mwaka pamoja," alisema


Onesho la usiku wa Fm Academia utakaofanyika katika ukumbi wa Aventure, ulioko Majengo mjini hapa kwa kiingilio cha shilingi 10,000, unadhaminiwa na kinywaji cha Windhoek Lager.

No comments:

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...