Meneja wa TANROAD mkoa wa
Kilimanjaro, Marwa Rubirya akizungumza na Washiriki katika ufunguzi wa Semina
hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa Kiliamnajro Cranes kutoa mafunzo ya
ushirikishwaji wa wanawake katika kazi za Barabara nchini.
Kaimu katibu Tawala wa Mkoa wa
Kilimanjaro, Martha Ufunguo, akizindua semina ya mafunzo ya siku kumi kwa
Washiriki zaidi ya 30 yaliyoandaliwa na Wizara ya Ujenzi kutoa mafunzo ya
ushirikishwaji wa wanawake katika kazi barabara, yaliyofanyika leo katika
ukumbi wa Kilimanjaro Cranes, mkoani Kilimanjaro.
Mratibu wa Wizara ya Ujenzi,
Mhandisi Mwanaisha Urenge, akizungumza na Washiriki zaidi ya 30 katika semina
ya mafunzo ya ushirikishwaji wa wanawake katika kazi barabara, yaliyofanyika
leo katika ukumbi wa Kilimanjaro Cranes, mkoani Kilimanjaro.
Katika picha ya pamoja ni washiriki
wa semina ya siku ya mafunzo ya ushirikishwaji wa wakandarasi wanawake katika
kazi za barabrani, kutoka katika mikoa ya Kilimanjaro, Tanga, Geita, Manyara,
Arusha, Singida, Da es salaam, Katavi na Pemba, yaliyoandaliwa na Wizara ya
Ujenzi, katikia ukumbi wa Kilimanjaro Cranes, Mkoani Kilimanjaro.
Katika picha ya pamoja ni washiriki
wa semina ya siku ya mafunzo ya ushirikishwaji wa wakandarasi wanawake katika
kazi za barabrani, kutoka katika mikoa ya Kilimanjaro, Tanga, Geita, Manyara,
Arusha, Singida, Da es salaam, Katavi na Pemba, yaliyoandaliwa na Wizara ya
Ujenzi, katikia ukumbi wa Kilimanjaro Cranes, Mkoani Kilimanjaro.
Na Mwandishi Wetu, Kilimanjaro
WIZARA ya Ujenzi imetoa
mafunzo kwa wanawake wakandarasi kuhusu njia ambayo inaweza kuwasaidia
kushiriki kikamilifu katika kazi za ujenzi za Barabara ambapo imebainika kwamba
wanawake wengi wakandarasi hukumbana na changamoto nyingi katika kazi za ujenzi
kutokana na uwepo wa ushindani mkubwa kwa sasa.
Hayo yamebainishwa leo katika semina
ya mafunzo ya Wizara ya Ujenzi, Barabara na Nyumba na kutoa uwezo kwa wahandisi
wanawake kushiriki kikamilifu katika kazi za barabarani yaliyofanyika katika
ukumbi wa Kilimanjaro Cranes na kushirikisha washiriki zaidi ya 30 kutoka
katika mikoa zaidi kumi.
No comments:
Post a Comment