Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
BAADA ya kutokea vuta
nikuvute kati ya wagombea wa nafasi mbalimbali za Uongozi wa Shirikisho la Soka
Tanzania (TFF) na kamati ya uchaguzi, wagombe waliokatwa majina yao katika
mchakato huo sasa huenda wakawa na nafuu baada ya mchakato wote kuanza upya.
Rais wa TFF, Leodgar Tenga
Akizungumza na
Waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Rais wa TFF Leodger Tenga amesema
kwamba mchakato wa kuwapata viongozi hao utaanza upya Oktoba mwaka huu.
Tenga alisema kwamba
uamuzi wa kuanza upya kwa zoezi la uchaguzi huo umeamuliwa na Shirikisho la
Soka duniani (FIFA) na kwamba mchakato wa kuchukua fomu utatangazwa upya na
wagombea wote kufanyiwa mchujo kama ilivyokuwa hapo awali.
Zoezi la Uchaguzi huo
uliingia doa baada ya Kamati ya Uchaguzi kuondoa majina ya wagombea wawili,
Jamal Malinzi na Michael Wambura katika kuwania nafasi walizokuwa wakipigania, huku wakionyeshwa kuungwa mkono na watu wengi.
No comments:
Post a Comment