Na Mwandishi Wetu, Dodoma
BUNGE kwa kupitia Waziri wa
Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera na Uratibu wa Bunge, William Lukuvi, leo
ametangaza uamuzi uliochukuliwa na Tume ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda, kufuatia
mtihani wa kidato cha nne mwaka 2012 watoto wengi kufeli.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera na Uratibu wa Bunge, William Lukuvi
Kwa mujibu wa Tume hiyo,
imependekeza mtihani wa kidato cha nne kusahihishwa upya huku ikiyafuta yale
yaliyotangazwa kwa ajili ya kuweka usahihi na njia ya kuelekea kilele cha ubora
wa elimu ya Watanzania wote.
Akizungumza Bungeni leo mjini
Dodoma, Lukuvi alisema kuwa mitihani hiyo inapaswa kusahihishwa kwa kufuata
kanuni ya mwaka 2011, hivyo uamuzi huo umetolewa na Tume ya Waziri Mkuu Pinda
aliyounda baada ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kutangaza matokeo ya
kidato cha nne huku asilimia 60 ya wanafunzi wote kufeli.
Suala hilo liliibua mtafaruku
mkubwa kwa wadau na wanasiasa wa Tanzania, wakililia haki ya mtoto wa Tanzania
kusoma, huku wakisema kufeli kwao kutaongeza joto la maisha magumu kwa watoto
hao ambao wengi wanatoka kwenye familia masikini.
Taarifa zaidi ya Tume hiyo na
uamuzi wako itaendelea kukujia katika blog yako hii, kwa ajili ya kukufikishia
habari kamili na namna ya kuwapatia haki ya kupata elimu watoto wa Tanzania.
No comments:
Post a Comment