https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543


Recent Post

Wednesday, May 01, 2013

CUF: Watoto wadogo wabambikiwa kesi ya unyang'anyi wa kutumia silaha Liwale, mkoani Lindi



Kutoka kwa Julius Mtatiro-CUF
WATOTO Sais Hassan Badi miaka 14 na Salma Hashim Mbwana (14) wote wanafunzi wa kidato cha kwanza wamefikishwa mahakama ya wilaya ya Liwale na kusomewa mashtaka kwenye kesi zaidi ya tatu.
 Naibu Katibu Mkuu wa CUF Tanzania Bara, Julius Mtatiro, akizungumza na watoto waliobambikiwa kesi mjini Liwale.



Naibu Katibu Mkuu wa CUF Tanzania Bara, Julius Mtatiro, akizungumza na watoto waliobambikiwa kesi mjini Liwale.


Naibu Katibu Mkuu wa CUF Tanzania Bara, Julius Mtatiro

Kwa mujibu wa Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi (CUF), Julius Mtatiro, katika kesi moja watoto hawa wanatuhumiwa kuvamia duka, kulivunja, kuona na kumtishia mwenye duka (mwanaume) watamuua kwa silaha.
Nilipoongea na watoto hawa nilishangaa sana, huyo wa kiume anasema siku ya matukio ya wananchi kufanya vurugu yeye alikuwa anaangalia mpira, aliposikia milio ya risasi majira ya jioni alikimbia kutoka ukumbini, njiani akakutana na mjomba wake ambaye ni diwani wa CCM, mjomba wake akamuuliza anakimbia nini?

Akamjibu kuwa ameambiwa kuwa kuna vurugu hivyo anakimbilia nyumbani.

Diwani wa CCM akamwambia anawajua vijana waliomjulisha kuhusu vurugu? Kijana huyu akajibu hawajui, ndipo mjomba mtu(diwani) akaanza kumpiga makofi, na mwisho wa siku kijana huyu akakimbilia kwao.

Keshoye akaamkia shuleni, akiwa shuleni mjomba wake akaja na polisi, wakamkamata. Hajui lolote kuhusu matukio hayo lakini anasomewa shtaka la kuona kwa kutumia silaha usiku wa manane.

Huyu SALMA(msichana), anasema siku moja baada ya matukio ya LIWALE, polisi walifika nyumbani kwao(Yeye Salma na mama yake wanasimamia nyumba ya ndugu yao yenye wapangaji). Polisi walipofika wakamkamata mpangaji mmoja na kusachi chumba cha mpangaji huyo. Baadaye polisi wakaondoka na mpangaji huyo pamoja na DRYER ya Saloon na kiti cha Saloon(vinavyosemekana kuwa vya wizi).

Baada ya muda kidogo, polisi wakarudi na wakaanza kumpiga sana msichana huyu na mama yake, wakawakamata na kuwaweka Rumande. Yule mpangaji alokutwa na vitu vya wizi aliachiwa kesho yake na hajapandishwa kizimbani.

Hadi mtoto huyu na mama yake wanafikishwa mahakamani hawakuwahi kujua kosa lao ni nini.
 
Wamefikishwa mahakamani na kushtakiwa kwa kesi 4 tofauti. Katika kesi mojawapo, mtoto huyu anatuhumiwa kwa kesi ya unyang'anyi wa kutumia silaha na haina dhamana.

Chama kimechukua hatua za dharura za kuweka mawakili ili wananchi wanaobambikiziwa kesi wanusurike. Inasikitisha sana. Polisi watumika vibaya. Habari hii na picha zote ni kwa hisani ya Julius Mtatiro

No comments:

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...