Baadhi ya wachezaji wa Kilimanjaro Stars, wakishangilia ushindi uwanjani. Hata hivyo, timu hiyo haijafanikiwa kuwapoka Uganda Kombe hilo kwa mwaka wa pili mfululizo.
Na Kambi Mbwana, Handeni
TIMU ya Taifa, (Kilimanjaro Stars)
iliyokuwa inashiriki michuano ya Kombe la Chalenji jijini Kampala, nchini
Uganda, inarejea leo jioni jijini Dar es Salaam, nchini Tanzania.
Kwa mujibu wa taarifa ya Ofisa
Habari wa Shirikisho la Soka nchini (TFF), Boniface Wambura, timu hiyo itatua
Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) saa 11 kamili jioni kwa
ndege ya Precision Air.
Wambura alisema baada ya Kilimanjaro
Stars na Zanzibar Heroes kumaliza kushiriki mashindano ya Kombe la Chalenji
jijini Kampala, Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Kim Poulsen kesho Jumatatu (Desemba
10, 2012) saa 6 kamili mchana ofisi za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania
(TFF) atatangaza kikosi chake kitakachoingia kambini jioni ya Desemba 12, 2012
jijini Dar es Salaam kujiandaa kwa mechi ya kirafiki dhidi ya mabingwa wa
Afrika, Zambia (Chipolopolo) itakayofanyika Desemba 22, 2012 katika Uwanja wa Taifa.
Katika mashindano ya Chalenji
yaliyomalizika nchini Uganda, timu ya Taifa ya Uganda ilifanikiwa kutwaa
Ubingwa huo kwa mara ya pili mfululizo.
No comments:
Post a Comment